Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Nchi za Magharibi zaongeza vikwazo dhidi ya Urusi

Urusi ilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Ukraine mnamo Alhamisi, Februari 24, ambapo nchi za Magharibi zimejibu kwa vikwazo vipya.

Wakikutana katika mkutano wa kilele Alhamisi hii jioni, Februari 24, viongozi wa Ulaya waliidhinisha mlolongo mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.
Wakikutana katika mkutano wa kilele Alhamisi hii jioni, Februari 24, viongozi wa Ulaya waliidhinisha mlolongo mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi baada ya uvamizi wake nchini Ukraine. AP - Olivier Hoslet
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Rais wa Marekani Joe Biden alihutubia taifa Alhamisi jioni. Vladimir Putin atakuwa "atatengwa katika eneo la kimataifa," alisema katika mkutano na waandishi wa habari kutoka Ikulu ya White House. Ikiwa Marekani haitatuma wanajeshi Ukraine, inaendelea kuichukulia hatua kali Urusi.

Mamlaka ya Marekani imelenga benki mbili kubwa nchini humo, Sberbank na VTB Bank. Kampuni kubwa ya nishati ya Gazprom na makampuni mengine makubwa nchini -  kwa jumla taasisi 13 - hazitaweza tena kukusanya pesa kwenye masoko ya fedha ya Magharibi. Adhabu ambayo tayari ilikuwa imechukuliwa dhidi ya serikali ya Urusi yenyewe.

Kwa upande wa rais wa Marekani amesema, "vikwazo ambavyo tunaweka kwa benki vina athari sawa hata labda ya athari muhimu zaidi kuliko kusimamishwa kwa Swift. Halafu huwa ni chaguo lakini tunapozungumza sio uamuzi ambao Ulaya yote wanataka kufanya. Vikwazo tueka vinaenda mbali zaidi kuliko ambavyo vimewahi kufanywa. Vikwazo hivi vimesababisha theluthi mbili ya dunia kuungana nasi. "

Lakini vikwazo hivi haviendi mbali kama baadhi ya waangalizi walivyotarajia. Hasa, wanaepuka kuitenga Urusi kutoka kwa mtandao wa benki ya Swift, ambayo inafanya uwezekano wa kupokea au kutuma malipo duniani kote. Hili lingeinyima nchi uwezo wake wa kuondoa mapipa yake ya mafuta kwa urahisi, chanzo kikuu cha mapato. Hatua hii daima ni "chaguo", hata hivyo amesisitiza rais wa Marekani.

Vikwazo "vikubwa" vya EU

Wakikutana katika mkutano huo, viongozi wa Ulaya pia waliidhinisha vikwazo "vikubwa" dhidi ya Urusi, bila hata hivyo kwenda mbali na kuiondoa nchi hiyo kutoka kwa mfumo wa benki wa kimataifa wa Swift. "Viongozi wa Urusi watakabiliwa na vikwazo vikali," ameahidi Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen. Hii ni "seti ngumu zaidi ya vikwazo kuwahi kutekelezwa" na Umoja wa Ulaya, alisema Mkuu wa sera ya Mambo ya Nje wa Ulaya Josep Borrell.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapiga kura leo Ijumaa juu ya azimio ambalo litalaani uvamizi wa kijeshi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Baraza hilo la Usalama pia kwa kauli Kali litaitaka Urusi kusitisha uvamizi dhidi ya Ukraine na kuwaondoa wanajeshi wake mara moja. Azimio hilo lilipitishwa haraka hapo jana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 wasio na kura ya turufu. Dhamira ya Baraza Kuu la Umoja wa Matafa ni kudumisha uhuru, umoja, na uadilifu wa kuheshimu maeneo ya Ukraine yaliyo ndani ya mipaka yake inayotambulika kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.