Pata taarifa kuu

IMF yaonya juu ya kiwango cha juu cha deni la kimataifa

Ingawa deni la kimataifa na la kibinafsi lilirekodi kupungua mnamo 2022, bado liko juu ya kiwango cha kabla ya janga la Uviko-19: dola za kimarekani trilioni 235, au 238% ya pato la jumla la kimataifa. Hii ni pointi 9 zaidi ya mwaka wa 2019.

Kulingana na IMF, deni la kimataifa la umma na la kibinafsi limefikia 238% ya pato la taifa mwaka 2023, sawa na pointi 9 zaidi kuliko mwaka wa 2019.
Kulingana na IMF, deni la kimataifa la umma na la kibinafsi limefikia 238% ya pato la taifa mwaka 2023, sawa na pointi 9 zaidi kuliko mwaka wa 2019. REUTERS - Johannes Christo
Matangazo ya kibiashara

Kuna sababu kadhaa za deni hili kupita kiasi. Kuchukua faida ya viwango vya chini vya riba, vilivyoanzishwa baada ya mgogoro wa kifedha wa mwaka 2008, serikali lakini pia wafanyabiashara na kaya wamechukua madeni makubwa. Sababu nyingine; Wakati wa janga la Uviko-19, mataifa yalipitisha hatua za usaidizi wa kibajeti ili kukabiliana na kushuka kwa ghafla kwa shughuli za kiuchumi na kuendeleza ukuaji. Kisha ukaja mfumuko wa bei, ambao ulishika kasi kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine; serikali nyingi zimetumia zaidi kukabiliana na kupanda kwa bei ya vyakula na nishati. Hatua hizi zote zilifadhiliwa na deni ambalo, kwa hiyo, lilikuwa kiongezeka.

Nchi tajiri zilizo na vifaa bora vya kukabiliana na mzozo huo

Matarajio ya mzozo wa kifedha ni mdogo katika nchi zilizoendelea, ambazo zina mifumo thabiti ya usimamizi, nafasi ya kujilinda na benki kuu zenye uwezo.

Kwa upande mwingine, kuna hatari ya kweli kwa nchi zinazoendelea zenye mapato ya chini. “Deni la nchi hasa katika Afŕika, kwa mfano, limeongezeka zaidi ya maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Na tatizo ni kwamba kupanda kwa viwango vya riba kutoka kwa Hifadhi ya Shirikisho la Marekani kunaongeza thamani ya dola, jambo ambalo linaongeza moja kwa moja deni ambalo nchi za Afrika zinapaswa kulipa, kwa sababu zimechukua madeni mengi kwa dola,” anasema Thomas Grjebine , mkuu wa mpango wa uchumi mkuu katika Kituo cha Mafunzo Yanayotarajiwa na Habari za Kimataifa (CEPII). Kulingana na afisa huyo, "kati ya mwaka 2020 na 2023, kulikuwa na kasoro tisa za uhuru kati ya nchi hizi, hali ambayo ni rekodi".

Kwa hakika, kulingana na Shirika la Fedha Duniani (IMF), deni la nchi zinazoendelea limeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miongo miwili iliyopita. Kulingana na taasisi hiyo yenye makao yake makuu mjini Washington, zaidi ya nusu ya nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini zinakabiliwa na deni. Deni linalozinyonga nchi hizi na kuzuia maendeleo yao ya kiuchumi. Hali iliyoshtumiwa na Umoja wa Mataifa: "Mgogoro wa madeni ni janga kwa nchi maskini," alishutumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guetteres wakati wa majira ya joto. Alisema ubinadamu unaishi katika nchi ambazo hutumia zaidi ya riba ya deni kuliko elimu au afya.

IMF inaonya hasa juu ya kiwango cha juu cha deni nchini China

Deni la China lilifikia karibu 272% ya Pato la Taifa mwaka jana. Kulingana na IMF, Ufalme wa Kati umekuwa na jukumu kuu katika kuongeza deni la kimataifa katika miongo ya hivi karibuni, kwani ukopaji wake umepita ukuaji wa uchumi. Hakika, ili kufadhili ukuaji wake mkubwa wa uchumi, serikali ya China pamoja na wafanyabiashara na mahiriika ya aumma wameingia kwenye deni kubwa katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.

Kutokana na uchunguzi huu, IMF kwa mara nyingine tena inatoa wito kwa viongozi wa kisiasa duniani kote "kuchukua hatua za haraka za kubadili mkondo wa madeni wa muda mrefu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.