Pata taarifa kuu

IMF kuipa Argentina msaada wa dola bilioni 7.5

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetangaza kuwa limefikia makubaliano mapya na Argentina. Argentina ambayo ina mzigo mkuwa wa deni na ambayo inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni, itapokea deni lenye thamani ya dola bilioni 7.5 kutoka kwa shirika la kifedha mnamo mwezi Agosti. Hali ambayo itarejesha afueni katikaa uchumi  wa nchi hiyo.

Noti za dola na peso huko Buenos Aires, Argentina.
Noti za dola na peso huko Buenos Aires, Argentina. AP - Victor R. Caivano
Matangazo ya kibiashara

Deni hili la dola bilioni 7.5 litafanya uwezekano wa kunusuru hazina ya Benki Kuu ya Argentina, ambayo kwa sasa iko hali ya kutatanisha.

Ukosefu wa fedha za kigeni si jambo geni kwa Argentina, lakini ulichochewa mwaka huu na ukame wa kihistoria ambao ulisababisha Buenos Aires kupoteza zaidi ya dola bilioni 20 katika mapato ya mauzo ya nafaka. Kwa kuzingatia hali hii ya kipekee, na ili nchi iweze kutimiza ahadi zake za kimataifa, Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limekubali kuipa mara moja serikali ya Argentina fedha amazo ingeliipa hadi mwisho wa mwaka 2023.

Utoaji huu mpya wa fedha sasa unafikisha dola bilioni 36.3 jumla ya kiasi cha fedha ambacho tayari kimetengewa kwa Argentina tangu kuanza kwa mpango wa usaidizi mwezi Machi 2022. Makubaliano haya ya 2022 ni makubaliano ya 13 kati ya IMF na nchi hii ya Amerika Kusini tangu 1983. Kwa jumla, mpango wa miezi 30 unapaswa kutoa jumla ya msaada wa dola bilioni 44 [au takriban SDRs bilioni 32.

Miezi mitatu kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, serikali ya Argentina inatumai kuwa mkataba huu na IMF utafanya uwezekano wa kuleta utulivu wa hali ya kiuchumi ya jadi katika kipindi cha kabla ya uchaguzi.

IMF inatarajia ukuaji wa 0.2% tu kwa 2023, na mfumuko wa bei unatarajiwa kupungua kwa kiasi fulani mwishoni mwa mwaka, hadi 88%. Hata hivyo, mfumuko wa bei ulifikia 115.6% kwa kiwango cha mwaka mwezi Juni, kulingana na data kutoka Taasisi ya Taifa ya Takwimu (INDEC).

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.