Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Makombora ya Urusi yautikisa mji mkuu wa Kiev

Jioni ya siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Rais wa Ukraine Zelensky aliripoti idadi ya vifo vya watu 137 na akasikitika kwamba nchi yake iliachwa "peke yake dhidi ya Urusi".

Maafisa wa Wazima moto wakijaribu kuzima moto baada ya shambulio la anga la jeshi la Urusi katika eneo la makazi la Kiev, Ukraine, Februari 25, 2022.
Maafisa wa Wazima moto wakijaribu kuzima moto baada ya shambulio la anga la jeshi la Urusi katika eneo la makazi la Kiev, Ukraine, Februari 25, 2022. © REUTERS/UKRAINIAN MINISTRY OF EMERGENCY
Matangazo ya kibiashara

Uhamasishaji wa jumla umesikika nchini humo kujaribu kuzuia mashambulizi makubwa yaliyoanzishwa na Vladimir Putin, ambayo Marekani na Umoja wa Ulaya wamejibu kwa hatua mpya za vikwazo. Shambulio kubwa katika mji mkuu wa Kiev linahofiwa kutokea kwa saa chache zijazo.

Pointi kuu:

► Ijumaa hii, macho yote kwa sasa yanaelekezwa katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev ambako "makundi ya hujuma" ya Urusi yanaendesha ukatili kwa sasa, kulingana na rais wa Ukraine Alhamisi jioni, ambaye alisema alikuwa "mlengwa namba moja" kwa mashambulizi ya Moscow. Jeshi la Urusi linakaribia mji mkuu Kiev.

► Siku ya Alhamisi, siku ya kwanza ya uvamizi wa Urusi, Kremlin ilidai "mafanikio" baada ya kuzima au kuchukua udhibiti wa maeneo mengi ya kimkakati, ikiwa ni pamoja na kituo cha nyuklia cha Chernobyl. Pia Urusi imetangaza kwamba waasi wanaotaka kujitenga wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine wamepata mafanikio makubwa. Mapigano yanaendelea katika maeneo mengi ya nchi.

► Majeshi ya Urusi, hata hivyo, yalichukua udhibiti wa Chernobyl, eneo la maafa ya nyuklia ya 1986 na mahali ambapo bado kuna mionzi hadi leo - na kusababisha wasiwasi mkubwa kutoka kwa walinzi wa nyuklia wa kimataifa.

► Idadi ya vifo iliyotolewa Alhamisi jioni na rais wa Ukraine inaripoti kuwa watu 137 wameuawa na 316 kujeruhiwa katika mapigano. Hata hivyo, watu 100,000 kulingana na Umoja wa Mataifa, wametoroka nchi yao na kkimbilia nchi jirani kama vile Poland.

► Mkutano wa NATO utafanyika Ijumaa hii kwa njia ya video. Marekani italinda "eneo la NATO", lakini haitatuma wanajeshi wake Ukraine, ametangaza rais wa Marekani Joe Biden. Marekani imeamuru wanajeshi 7,000 wa ziada kwenda Ulaya.

► Mataifa ya Magharibi yameongeza vikwazo vya kifedha kwa benki za Urusi na maafisa wa ngazi za juu, huku Marekani ikikata mauzo ya teknolojia ya juu nchini Urusi - lakini mataifa ya Nato hayatatuma wanajeshi wake Ukraine.

► Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kuendelea na mapigano, akisema kuwa "pazia jipya la chuma" linaangukia mahali pake - na kazi yake ni kuhakikisha nchi yake inasalia upande wa magharibi.

► Maandamano ya kupinga vita na maandamano ya kuunga mkono Ukraine yamefanyika katika miji kote Ulaya - na pia nchini Urusi, licha ya ukandamizaji ambao umesababisha kukamatwa kwa watu zaidi ya 700.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.