Pata taarifa kuu

Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yauawa 40, Kiev yahadi kujihami

Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa nchini Ukraine Alhamisi asubuhi yamesababisha kufikia sasa vifo vya takriban watu 40, kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Masoko ya hisa yameanguka huku ulimwengu ukijiuliza nini kitatokea baadaye.

Magari ya kijeshi ya Ukraine yanapita karibu na eneo la Uhuru huko Kiev mnamo Februari 24, 2022.
Magari ya kijeshi ya Ukraine yanapita karibu na eneo la Uhuru huko Kiev mnamo Februari 24, 2022. © AFP/DANIEL LEAL
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza vita dhidi ya Ukraine, akitoa wito kwa jeshi la Ukraine kuweka silaha chini. Miji kadhaa ya Ukraine ilishambuliwa Alhamisi asubuhi. Ukraine imeahidi kujihami.

"Putin ameanzisha uvamizi, vita kamili dhidi ya Ukraine," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Urusi Vladimir Putin mwenyewe alitangaza operesheni ya kijeshi katika eneo la Donbass mashariki mwa Ukraine mapema Alhamisi saa za nchini Urusi.

Katika hotuba iliyotangazwa na televisheni ya taifa ya Urusi Alhamisi kabla ya saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Urusi, Putin alivitaka vikosi vya Ukraine kuweka chini silaha zao na kurejea nyumbani, akisema jukumu lolote la uwezekano wa umwagaji damu litaihusu serikali ya Ukraine; akiongeza: "Mipango yetu sio kudhibiti Ukraine, hatuna mpango wa kujilazimisha kwa mtu yeyote," CNN imeripoti.

Kiongozi huyo wa Urusi alidai kuwa Urusi ilikuwa ikifanya "operesheni maalum ya kijeshi" ili "kuondoa silaha" na "kuondo sera za kinazi" nchini humo kwa kisingizio kwamba Urusi ilikuwa ikijihami, kulingana na Gazeti la New York Post. Mara tu baada ya hotuba hiyo, milipuko iliripotiwa katika mji mkuu wa Kiev, Kramatorsk, Kharkiv, Odessa na Mariupol-- miji yote mikubwa nchini Ukraine.

"Mashambulizi yanaendelea katika miji yenye amani ya Ukraine. Ni vita vya uchokozi. Ukraine itajihami na kushinda. Ulimwengu unaweza na lazima umzuie Putin. Ni wakati wa kuchukua hatua - sasa hivi.” amesema Bw. Kuleba, akinukuliwa na Gazeti la New York Post.

"Ulimwengu lazima uchukue hatua mara moja. mustakabali wa Ulaya na ulimwengu uko hatarini", ameongeza.

Kwa upande wake, Vladimir Putin amehalalisha hatua yake kwa wito wa usaidizi anaodaiwa kupokea kutoka kwa viongozi wa maeneo yanayotaka kujitenga yanayoungwa mkono na Urusi yaliyoundwa mashariki mwa Ukraine mwaka 2014, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani.

"Nimechukua uamuzi wa kutekeleza operesheni maalum ya kijeshi. Lengo lake litakuwa ni kuwatetea watu ambao kwa miaka minane wameteswa na mauaji ya halaiki na utawala wa Kiev. Kwa hili, tutalenga kuiondoa Ukraine kijeshi pamoja na kufunguliwa mashtaka kwa wale ambao wamefanya uhalifu mwingi wa umwagaji damu dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na raia wa Shirikisho la Urusi. Mipango yetu haijumuishi uvamizi wa eneo la Ukraine," alisema Bw. Putin, akinukuliwa na Gazeti la New York Times.

Kisha mpangaji wa Kremlin alihutubia vikosi vya Kiukreni moja kwa moja, akiwahimiza kuweka silaha zao chini mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.