Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Zoezi la Kura za mchujo laanza New York

Nchini Marekani, wapiga kura wameanza zoezi la kuwapigia kura wanasiasa wa chama cha Republican na Democratic wanaowania tiketi ya vyama hivyo kuwania urais mwezi Novemba mwaka huu.

Hillary Clinton na  Donald Trump wakipewa na fasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa mchujo kupitia vyama vyao vya Democratic na Republican katika jimbo la New York, Jumanne April 19, 2016..
Hillary Clinton na Donald Trump wakipewa na fasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa mchujo kupitia vyama vyao vya Democratic na Republican katika jimbo la New York, Jumanne April 19, 2016.. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili ni muhimu kwa wanasiasa hao kwa sababu utabainisha ni nani maarufu kuelekea uteuzi wa ndani katika vyama hivyo.

Wadidisi wa siasa za Marekani wanasema, mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton anatarajiwa kumshinda mpinzani wake Bernie Sanders huku Donald Trump akinuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama..

Kwa wagombea wa chama cha Democtrats Bernie Sanders amelelewa mjini New York naye Hillary Clinton amekuwa seneta katika jimbo hilo.

Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.

Ted Cruz hivi karibuni alikosoa sera za Donald Trump kwenye kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.