Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Bunge kujadili "hali ya hatari" katika hali ya mvutano

Bunge la Venezuela linatazamiwa kujadili Jumanne hii uamuzi wa serikali wa kuongeza nguvu zake katika masuala ya usalama, wakati ambapo mvutano umeendelea kukua kati ya Rais Maduro na upinzani, ambao umetolea wito wafuasi wake kumiminika mitaani Jumatano wiki hii.

Maandamano dhidi ya Rais Nicolas Maduro Caracas, Venezuela, Mei 11, 2016.
Maandamano dhidi ya Rais Nicolas Maduro Caracas, Venezuela, Mei 11, 2016. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu usiku, nchi hii imepiga hatua kuelekea utawala wa udikteta wa baada ya Rais Nicolas Maduro kutoa tangazo la "hali ya hatari".

Sheria hii ya kirais iliyotolewa Jumatatu hii jioni inatoa siku 60 hadi kwa serikali kutumia uwezo wake katika suala la usalama na ugavi wa chakula: jeshi na polisi sasa vimepewa maelekezo ya "kuhakikisha kusimamia zoezi la usambazaji na uuzaji wa chakula na bidhaa mahitajio."

Kamati za usalama za wananchi, zilizowekwa hivi karibuni, zimepewa majukumu ya "usimamizi" na "kurejesha utulivu" na "kusimamia usalama na uhuru wa nchi."

Baadhi ya wataalam wamesema kuwa huo ni ukiukwaji katika suala la uhuru wa watu binafsi na wana hofu ya kutokea kwa makabiliano kati ya raia na vikosi vya usalama na ulinzi.

Hali hii inayoshuhudiwa nchini Venezuela inaweza kuwa kama ile iliyotokea nchini Brazil.

Wakati huo huo upinzani unaojumuika kwa jina la MUD, ambao una idadi ya wabunge wengi, unatazamiwa kujadili Jumanne hii hali hii ya hatari iliyotangazwa na Rais Maduro.

Katika nchi hii inazozalisha mafuta, ambayo ni yenye uchumi unaokumbwa na kuporomoka kwa bei ya mafuta ghafi, serikali iliendelea kutangaza hatua katika wiki za hivi karibuni kwa kukabiliana na mgogoro, unaochochewa kwa sasa na uhaba wa umeme.

Venezuela inakabiliwa mara kwa mara na kukatika kwa umeme kutokana na matukio mbali mbali ya hali ya hewa kama El Niño, ambayo imesababisha ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, serikali imesema.

Baadhi ya hatua zilizotangazwa zinashangaza: watumishi katika sekta ya umma wanatakiwa kufanya kazi Jumatatu na Jumanne kwa wiki. Na karibu nchibi kote (isipokuwa Caracas), umeme utakatwa angalau masaa manne kwa siku.

Hali hiyo ilisababisha wiki hii iliyopita yenye maandamano na ghasia katika mji wa Maracaibo (kaskazini magharibi mwa nchi), mji wa pili kwa ukubwa wenye wakazi milioni 1.5.

Tangu ushindi wa muungano wa upinzani katika uchaguzi wa bunge mwishoni mwa mwaka 2015, nchi hii tajiri kwa mafuta inakabiliwa na mzozo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, mgogoro ambao unaibua mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.