Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHUMI

Uchumi wa Zimbabwe waendelea kudidimia

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa, kuanzia mwezi ujao itatoa noti mpya ambazo zitakuwa sawa na dola ya Marekani, tangazo lililoibua hofu ya taifa hilo kurejea kwenye kipindi cha mfumuko mkubwa wa bei uliosababisha uchumi wa taifa hilo kuharibika, miaka michache iliyopita.

Uamuzi wa viongozi wa Zimbabwe unalenga kutafuta ufumbuzi kuhusu ukosefu wa fedha.
Uamuzi wa viongozi wa Zimbabwe unalenga kutafuta ufumbuzi kuhusu ukosefu wa fedha. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo linaloongozwa na kiongozi mkongwe zaidi barani Afrika, Comrade Robert Gabriel Mugabe, lilitangaza kuanza kutumia dola ya Marekani na Randi ya Afrika Kusini mwaka 2009, baada ya nchi yake kukumbwa na hali mbaya ya uchumi iliyosababishwa na mfumuko wa beo uliofikia asilimia bilioni 500, hali iliyofanya Dola ya Zimbabwe kutokuwa na thamani.

 

Nchi ya Zimbabwe imekaukiwa na dola ya Marekani kwenye miezi ya hivi karibuni, ambapo inatarajiwa kupunguza makali yaliyopo ya uhaba wa fedha kwa kuchapisha fedha yake yenyewe mfano wa dola, ambapo itatoa dola mpya iakayoanzia na thamani ya dola 2 hadi 5.

Mpango huu wa Serikali hata hivyo tayari umesababisha ukosolewaji mkubwa toka kwa wataalamu wa masuala ya uchumi, ambao wanaona kuwa fedha hii mpya kamwei haiwezi kufikia thamani ya dola ya Marekani, na kwamba zaidi itaonekana ni kama toleo jipya la dola ya Zimbabwe iliyokufa na kupoteza thamani.

Serikali kupitia gavana wa benki kuu ya Zimbabwe. John Mangudya, amesema dola hiyo mpya ya Zimbabwe itaanza kutumika kuanzia mwishoni mwa mwezi wa 1

Kwa wiki kadhaa, Zimbabwe imekuwa ikikumbwa na wimbi la maandamano dhidi ya Robert Mugabe anayestumiwa kuwa chanzo cha wa mgogoro wa kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.