Pata taarifa kuu
URUSI

Urusi imetaka uchunguzi kuhusu vifo vya waandishi wa habari kufanyika

Serikali ya Urusi imetaka kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu vifo vya waandishi wa habari wawili wa kituo kimoja cha televisheni nchini humo, waliouawa mashariki mwa nchi ya Ukraine kwenye maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wenye silaha.

Raisi wa Urusi Vladmir putin
Raisi wa Urusi Vladmir putin AFP
Matangazo ya kibiashara

Tamko hili la Urusi linatolewa wakati huu ambapo, siku ya Jumanne ya wiki hii, rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenzake wa Ukraine, Petro Poroshenko wamefanya mazungumzo kujaribu kupata suluhu ya mzozo unaoendelea nchini Ukraine.

Viongozi hawa wamezungumzia uwezekano wa kusitishwa mapigano kwa muda kwenye baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo kuruhusu wananchi kuondoka kwenye maeneo hayo.

Katika hatua nyingine waziri mkuu wa Ukraine Arseny Iatseniouk ameamuru usalama uimarishwe kwenye eneo lenye mabomba ya gesi, baada ya waziri wa mambo ya ndani kusema kwamba kulitokea mripuko katika mojawapo ya mabomba hayo, ambao vyombo vya dola vinasema ulisababishwa na bomu.

Maafisa wa polisi wamethibitisha kuwa mripuko huo ulitokea jana katika mkoa wa Poltava kwenye bomba linalosafirisha gesi kwenda Ulaya.

Msemaji wa polisi amesema mripuko huo haukuathiri usafirishaji wa gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.