Pata taarifa kuu
UFARANSA-ISIL-Usalama-Haki za binadam

Raia wa Ufaransa waendelea kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam

Wanawake ambao ni raia wa Ufaransa walio kati ya 100 na 150 walijiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam tangu mwaka 2012. Mwishoni mwa mwezi wa Agosti familia moja ilikyokuaikiishi katika kati ya Ufaransa katika mji wa Vienne ilitoroka maakazi yake na kujielekeza nchini Syria.

Wanawake kati ya 100 na 150 raia wa Ufaransa wamejiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam au kundi la Al-Nosra (picha), lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda tangu mwaka 2012.
Wanawake kati ya 100 na 150 raia wa Ufaransa wamejiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam au kundi la Al-Nosra (picha), lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda tangu mwaka 2012. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Inasadikiwa kuwa familia hiyo ilienda kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam.

Wanawake wamekua wakishirikiana na waume zao kwa kujielekeza kwenye sehemu za mafunzo ya makundi hayo wakiwabeba watoto zao, wakiwemo watoto wachanga. Kuna hata wanawake wengine ambao si waolewaji wamekua wakijiunga na makundi hayo ya wapiganaji wa kiislam baada ya kuahidiwa kuolewa na mume kutoka wapiganaji hao wakiislam. Lakini wanawake hao washiriki katika vita.

Lengo la familia hizo ni kuunda jamii yenye kufuata sheria ya kislam. Kwa mujibu wa mmoja wa wanawake hao waliyehojiwa na RFI, “watoto wamekua wakipelekwa kwenye maeneo hayo ya wapiganaji ili wapate malezi yenye misingi ya kijihad”.

Viongozi wa mji wa Vienne wanashuku kwamba familia moja ilijiunga hivi karibuni na wapiganaji wa kiislam, huku ikiwa iliwapeleka wasichana wao watu, mmoja akiewa na umri wa miaka 3 na mwengine umri wa miaka 5 akiwemo mtoto mchanga, mwenye umri wa mwezi mmoja na nusu. Kwa mujibu wa vyombo vya sheria vya Ufaransa, Eddy mwenye umri wa miaka 34 ambaye aliingia Uislam pamoja na mkewe ,Jihane waliondoka Ufaransa mwishoni mwa mwezi Agosti.,

Taarifa za watu hao kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam zimekua zikitolewa na familia aidha watu walio karibu nao. Mke wa zamani wa Eddy, akitiwa hofu na usalama wa msichana wake ambaye alikua likizoni kwa baba yake, amefungua mashtaka, huku uchunguzi ukianzishwa, na tayari hati ya kukamatwa Eddy imetolea na vyombo vya sheria vya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.