Pata taarifa kuu
ULAYA-ISRAEL-PALESTINA-HAMAS-SHERIA

Israeli yailaumu Mahakama ya Ulaya

Israel imelani vikali uamuzi wa Mahakama ya Ulaya ya kuondoa Hamas katika kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi kwa sababu ya hitilafu za kiutaratibu.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akinyooshea kidole cha lawama Mahakama ya Umoja wa Ulaya.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akinyooshea kidole cha lawama Mahakama ya Umoja wa Ulaya. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Orodha hii nyeusi iliwekwa baada ya mashambulizi ya Septamba 11 mwaka 2001 nchini Marekani. Kuna makundi mengi yanayojihusisha na ugaidi, ambayo yaliwekwa kwenye orodha hiyo, kama Hamas na tawi lake la kijeshi, ambavyo vilihusika na mashambulizi yaliyowalenga raia wa kawaida wa Israel.

Akihojiwa na RFI, mwanadiplomasia wa Ulaya mjini Brussels amesema kuwa hakuna mtu aliye unga mkono uamuzi wa Mahakama hiyo ambao umeibua utata.

Tume ya Umoja wa Ulaya imebaini kwamba itaendelea kuichukulia Hamas kama kundi la kigaidi na kubaini kwamba uamuzi wa Mahakama ya Ulaya uliyochukuliwa Jumatano wiki hii hauleti mabadiliko yoyote kwa msimamo wa kisiasa wa nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya umesema utakata rufaa ndani ya miezi mitatu, na kwa wakati huo, mali ya kundi hilo la Hamas zitaendelea kuzuiliwa.

Mashambulizi ya miaka 1990 na 2000 ndio yalipelekea Hamas kuwekwa kwenye orodha ya Umoja wa Ulaya ya makundi ya kigaidi . Nchi za magharibi haziungi mkono Hamas, licha ya ushindi wake katika uchaguzi wa wabunge uliyofanyika mwaka 2006.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi viliiwekea Hamas masharti matatu ili iweze kuwa mshirika wao wa karibu. masharti hayo ni pamoja na kuachana na vurugu, kuitambua Israeli na kutambua mikataba iliyoafikiwa kati ya Israel na Palestina. Masharti ambayo Hamas ilifutilia mbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.