Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-UFARANSA-URUSI-CHINA-UJERUMANI-UINGEREZA-NYUKLIA-DIPLOMASIA

Mpango wa nyuklia wa Iran: Kerry yuko tayari “kusitisha” mazungumzo

Baada ya mkutano wa mawaziri muhimu wa mambo ya nje wa nchi zenye nguvu duniani Alhamisi Julai 9 asubuhi mjini Vienna, nchini Austria, mazungumzo yameendelea kwa siku nzima na yangelipaswa kuendelea usiku mzima, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametangaza kuwa yuko tayari kusitisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametangaza kuwa yuko tayari kusitisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Matarajio yanayoweza kuathiri uchunguzi wa haraka wa mkataba kwa Baraza la wawakilishi la Marekani. Mbaya zaidi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani ameonya akisema kuwa yuko tayari "kusitisha" mazungumzo.

Mazungumzo yanaendelea kwa kasi mjini Vienna ili kufikia makubaliano, na wadau katika mazungumzo hayo wamekua wakizungumza kwa simu katika mkutano mapema leo Ijumaa asubuhi kati ya wahusika wakuu mbalimbali kutoka nchi tano zenye nguvu duniani (Marekani, Uingereza, Urusi, China, Ufaransa na Ujerumani) pamoja na Iran.

Mazungumzo hayo yanaweza hata kuendelea hadi usiku kucha. Laurent Fabius, ambaye ambaye amethibitisha kuwa " kuna matatizo ambayo bado ni vigumu kuyatatua ", hata kama " mambo yamefikia katika hatua nzuri ".

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa pia amesema: " Katika mazingira haya, nimeamua kukaa ili nifanye kazi usiku wa leo na kesho asubuhi na natumaini kwamba tutakuwa na uwezo wa kupatia ufumbuzi matatizo ambayo yanasalia". Maneno madogo ambayo yana madhara katika Atlantiki. Makubaliano ambayo yatatiliwa saini katika masaa yajao bila haka huenda yakaweza kuruhusiwa kufanyiwa uchunguzi wa haraka na Bunge la Congress la Marekani.

Baada ya siku nzima ya mazungumzo, ambayoJohn Kerry ameitaja kama "siku isiyo na kikomo," waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amethibitisha kuwa kuwa "hatuwezi kukimbilia kwenye makubaliano", na kuhakikisha kuwa matarajio ya makubaliano yanaonekana kuwa yako mbali. Kerry amesema pia kuwa yuko tayari, kama itahitajika, " kusitisha " mazungumzo. "Tupo hapa kwa sababu tunafikiri kufanya maendeleo halisi", amesema, huku akiongeza: " Hatutokubali kushinikizwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.