Pata taarifa kuu
URENO-SOARES

Rais wa zamani wa Ureno Mario Soares afariki dunia

Mario Soares ambaye anachukuliwa nchini Ureno kama Mwanademokrasia amefariki dunia Jumamosi hii Januari 7 akiwa na umri wa miaka 92, msemaji wa hospitali ya Lisbon ambapo alikuwa amelazwa amesema.

Mario Soares katika studio za RFI, mwaka 2013.
Mario Soares katika studio za RFI, mwaka 2013. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Mario Soares alilazwa hospitalini Desemba 13 akiwa katika hali mbaya. Afya yake ilidhoofika baada ya kifo cha mke wake mwezi Julai mwaka 2015. Baada ya ya matibabu ya muda mfupi, rais wa zamani wa Ureno alipoteza fahamu kwa muda mrefu toka Desemba 26, kufuatia " maradhi ambayo hayakuweza kutajwa.

"Mimi ni mtu wa kawaida"

Mwanzilishi wa chama cha Kisoshalisti nchini Ureno, Waziri wa Mambo ya nje, Waziri Mkuu mara mbili, rais kuanzia mwaka 1986 hadi 1996 na kisha Mbunge wa Ulaya, Mario Soares alikuwa kiongozi muhimu katika demokrasia ya Ureno.

"Mimi kamwe sijichukulii kama mtu wa ajabu. Mimi ni mtu wa kawaida," Mario Soares alisema katika mahojiano yaliyochapishwa mwezi Februari 2015. Mario Soares, mwanasheria aliye ingia katika siasa kama mpinzani katika utawala wa udikteta wa Antonio de Oliveira Salazar.

"Kuna watu ambao tayari wamesha endeleza na wataendeleza demokrasia yetu. Hatuna haja ya kuwa wale au kuwa katika chama kimoja na itikadi moja ili kutambua walichochangia kwa nchi hii, amesema rais Marcelo Rebelo Sousa, ambaye ni kutoka chama cha kihafidhina. "Kizazi changu kimeishi daima katika uhuru na uhuru huu tuliupata kupitia mikononi mwa Mario Soares", amesema Meya wa mji wa Lisbon, Fernando Medina ambaye ni kutoka chama cha Kisoshalisti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.