Pata taarifa kuu

[Moja kwa moja] "Operesheni ya kijeshi" nchini Ukraine: Habari za hivi punde

Alhamisi hii, Februari 24 alfajiri, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza "operesheni ya kijeshi" nchini Ukraine ambapo milipuko miikubwa ilisikika katika miji kadhaa, Kiev ikidai kuwa "uvamizi mkubwa" unaendelea.

Wakazi wa Kiev wakiondoka kwa magari baada ya Rais Putin kuidhinisha operesheni ya kijeshi mashariki mwa Ukraine.
Wakazi wa Kiev wakiondoka kwa magari baada ya Rais Putin kuidhinisha operesheni ya kijeshi mashariki mwa Ukraine. REUTERS - VALENTYN OGIRENKO
Matangazo ya kibiashara

Fuata habari zetu za hivi punde dakika baada ya dakika

Pointi kuu:

► Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza katika hotuba ambayo haikutangazwa kwenye televisheni mapema Alhamisi kwamba ameidhinisha operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

► Milipuko yenye nguvu imesikika katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na mji wa Kiev. Ving'ora vilisikika katika mji mkuu wa Kiev na mji wa Lviv.

► Jeshi la Urusi linahakikisha kwamba linalenga maeneo ya kijeshi ya Ukraine pekee. Moscow imedai kuharibu kambi za jeshi la wanaanga za Ukraine na mfumo wa ulinzi dhii ya mashambulizi ya anga, huku Kiev ikidai kudungua ndege tano za Urusi na helikopta moja.

► "Msiogope", "tutashinda", amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika hotuba yake kwa taifa. Ametangaza sheria ya kijeshi kote nchini.

► Mabalozi wa nchi 30 wanachama wa NATO wanatarajia kukutana haraka Alhamisi asubuhi huko Brussels.

► Ufaransa, kupitia rais wake Emmanuel Macron, imelaani vikali "uamuzi wa Urusi kuanzisha vita dhidi ya Ukraine". Rais wa Ufaransa aliitisha baraza la ulinzi saa tatu.

Raia wa Ukraine wameelezea wasiwasi wao kuhusu mashambulizi ya Urusi.

Wakati huo huo Ikulu ya Élysée imebaini kwamba imezungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye ametoa wito wa "umoja" kwa nchi za Ulaya.

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ataongoza mkutano kuhusiana na tukio hilo leo asubuhi ili kuamua juu ya "jibu" kwa "mashambulio ya kutisha" ya Urusi dhidi ya Ukraine, Ofisi ya Waziri mkuu, Downing Street, imetangaza.

Kwa upande mwengine serikali ya Poland imetangaza kwamba imeitaka NATO kuwezesha Kifungu cha 4 cha Mkataba wa Muungano, ambacho kinatoa mashauriano iwapo kutatokea tishio kwa usalama wa mojawapo ya wanachama. "Muda mfupi uliopita, balozi wa Poland huko Brussels aliwasilisha ombi kama hilo kwa Katibu Mkuu wa NATO, pamoja na kundi la washirika," msemaji wa serikali ya Poland Piotr Müller amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.