Pata taarifa kuu

Sweden na Denmark zatafuta kutunga sheria ili kuzuia udhalilishaji wa vitabu vitakatifu

Kwa ombi la Saudi Arabia na Iraq, mkutano wa usio kuwa wa kawaida unafanyika Jumatatu, Julai 31 huko Jeddah kati ya nchi za Jumuiya ya ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu (OIC) juu ya suala la kudhalilisha Quran nchini Sweden na Denmark. Katika miji ya Stockholm na Copenhagen, visa kama hivi vya kudhalilisha vitabu vya kidini vimepangwa kufanyika katika siku chache zijazo.

Mkimbizi wa Iraq Salwan Momika akiwa nje ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm ambako alikanyaga Quran, Julai 20, 2023.
Mkimbizi wa Iraq Salwan Momika akiwa nje ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm ambako alikanyaga Quran, Julai 20, 2023. AP - Oscar Olsson
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Stockholm, Carlotta Morteo

Denmark na Sweden zimetangaza kwamba zinatafuta suluhu za kisheria ili kukomesha visa hivi, ambavyo vimezua mvutano na nchi za utamaduni wa Kiislamu, pamoja na "hali ya hatari", kulingana na Sweden.

Serikali ya Denmark inasema itachunguza njia zote za kisheria ambazo zinaweza kufanya iwezekane kupiga marufuku baadhi ya maandamano ambayo huenda yakazua mambo mengine nchini humo. Hii kwa njia maalum kabisa, na bila kuathiri uhuru wa kujieleza unaolindwa na Katiba.

Ili kuhalalisha masuala yasiyokubalika kwa sheria hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark amekumbusha kwamba udhalilishaji huu unafanywa na "watu wachache", ambao lengo kuu ni "kuchochea chuki, kuleta mgawanyiko, kuwa na msimamo wa watu wenye itikadi kali".

Na sio tu tatizo la picha au sifa kwa Denmark, ameongeza Lars Lokke Rasmussen. Mkuu huyo wa diplomasia pengine alikuwa anarejelea hali iliyojitokeza katika miaka ya nyuma hususan kususia shughuli za serikali, vitisho vya kuuawa na mashambulizi yaliyozuiwa mwaka 2005, baada ya Gazeti la Denmark kuchapisha katuni za Mtume Muhammad.

Hali kama hiyo nchini Sweden: Stockholm pia inatafuta mfumo wa kisheria. "Hali ni hatari (..) kwa usalama wa taifa letu" aliandika Waziri Mkuu Ulf Kristersson Jumapili jioni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Hata hivyo, kongozi wa serikali ya Sweden anasema atakaa chini na mshirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia, chama cha Democrats cha Sweden, ambacho baadhi ya wabunge wake walitoa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu katika siku za hivi karibuni, kwa kushughulikia suala hilo.

Wakati huo huo, kulingana na kura za hivi punde, Wasweden na Wadenmark wanapendelea kwa kiasi kikubwa kupiga marufuku uchomaji wa vitabu hivi. Wakati huu huko Copenhagen na Stockholm, visa kama hivi vya kuchoma Quran vimepangwa kufanyika kuanzia Jumatatu na katika wiki zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.