Pata taarifa kuu

Wanamgambo wa Al Nusra Front wakashifu mashambulizi ya Marekani na washirika wake dhidi ya IS

Wapiganaji wa Al Nusra Front wa nchini syria wamekashifu mashambulizi yanayofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani na kusema hiyo ni vita dhidi ya uislamu.

Wapiganaji wa Al Nusra Front wasema Marekani imetangaza vita dhidi ya Uislamu
Wapiganaji wa Al Nusra Front wasema Marekani imetangaza vita dhidi ya Uislamu globalpost.com
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kupitia mtandao kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al qaeda lilitoa wito kwa wanajihadi wote duniani kukabiliana na mataifa ya magharibi na baadhi ya mataifa ya kiarabu yanayowapinga.

Hatua hiyo inakuja baada ya Marekani kuungana na mataifa mbalibali na kufanya mashambulizi dhidi ya wapiganajii wa dola la kiislamu nchini Iraq na Syria.

Idara ya usalama nchini Marekani imeeleza kuwa hapo jana shambulizi la anga lilitekelezwa katika mji wa Raqqa nchini Syria sambamba na katika kambi ya IS jirani na mpaka wa Uturuki.

Wapiganaji wa kikurdi wameendelea kuulinda mji wa kobane nchini Syria katika maeneo ya mpaka ili kuzuia uvamizi wa wapiganaji wa dola la kiislamu.

Muungano wa kijeshi wenye taribani nchi 40 unaosimamiwa na Marekani zikiwemo nchi za kiarabu zimejiapiza kukabiliana na kulitokomeza kundi la dola la kiislamu ambalo limedhibiti eneo kubwa kaskazini mashariki mwa Syria na kaskazini mwa Iraq.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.