Pata taarifa kuu
Tanzania

Tanzania kufuta usajili wa meli za Iran

Serikali ya Zanzibar nchini Tanzania imetangaza kufuta usajali wa meli za mafuta za Iran ambazo zimekuwa zikipeperusha bendera yake.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Uchukuzi katika kisiwa hicho Rashid Suleiman Seif amesema, walitapeliwa na mawakala ambao ni wauza mafuta huko Dubai na kuongeza kuwa wameshangazwa ni vipi meli hizo 36 zimekuwa zikitumia bendera yake.

Hatua ya Meli za Iran kutumia bedera za Tanzania kulimaanisha kuwa serikali ya Tehran ilikuwa inakwepa vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya wa kutouziwa mafuta yake kutokana na mpango wake wa nuclear.

Ijumaa iliyopita, Makamu wa rais wa Zanzibar aliliambia bunge la wawakilishi kuwa uchunguzi wao ulidhihirisha wazi kuwa ni kweli bendera za Tanzania zilikuwa zinaperushwa katika Meli za Iran.

Tanzania imechukua hatua hiyo ili kuepuka lawama au vikwazo vyovyote kutoka nchini Marekani na Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.