Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-Usalama

Wanajeshi wa Burundi waonekana katika ardhi ya Congo

Watu wenye kumiliki silaha wakivalia sare ya jeshi la Burundi wameone kana maeneo ya wilaya ya Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo karibu na mipaka ya Burundi na kuibua maswali kadhaa kuhusiana na utambulisho wao.

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, Lambert Mende, akikanusha kutokueko kwa wanajeshi wa Burundi katika aridhi ya Congo.
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, Lambert Mende, akikanusha kutokueko kwa wanajeshi wa Burundi katika aridhi ya Congo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni RFI imeshuhudia kuwepo kwa watu hao ambapo utata anendelea kuibuka kutoka kwa mashirika ya kiraia na wakazi wa maeneo hayo ambao kwa miezi kadhaa sasa wametaarifu kuwepo kwa askari wa jeshi la Burundi nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hata hivyo serikali za nchi hizo mbili za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinaendelea kukanusha kuhusiana na suala hilo.

Mwandishi wa RFI alijielekeza hivi karibuni katika kijiji cha Kiliba, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya ishirini kaskazini mwa mji wa Uvira na kilomita tano na mpaka wa Burundi.

Kwa mujibu wa mashahidi na mashirika ya kiraia mjini Uvira, watu kati ya 750 na 900 wenye silaha wakivalia sare za jeshi la Burundi wanaishi katika nyumba zaidi ya hamsini ziliyokua zikitumiwa kama maakaazi ya wafanyakazi wa kiwanda cha sukari, ambacho kwa sasa kimefungwa, na vile vile katika nyumba za tembe ziliyo sehemu mbili tofauti karibu na kijiji cha Kiliba.

Wakaazi wa kijiji cha Kiliba wamethibitisha kwamba wamekua wakiwaona wanajeshi hao katika kijiji hicho kila siku jioni wakipiga doria, huku magari yenye namba za usajili za Burundi yakionekana eneo hilo.

Inatosha tu kutembelea katika mashamba yaliyoko katika kijiji hicho kwenye umbali wa mita 500 na kuuona nyumba hizo za tembe na watu wakivalia sare za jeshi la Burundi.

Watu hao wanafanya nini sehemu hiyo? Hilo ni swali ambalo wakaazi wa Kiliba wamekua wakijiuliza. Hata hivyo Serikali za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia msemaji wake, Lambert Mende wamekanusha taarifa hiyo. Hata tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo Monusco imeielezea RFI kwamba taarifa hiyo haina ukweli wowopte. Monusco imebaini kwamba iliendesha uchunguzi na haikupata chochote.

Sasa watu hao ni akina nani? Je ni kikosi cha wanajeshi kutoka nchi jirani? Au ni vijana wa chama madarakani nchini Burundi Cndd-Fdd, Imbonerakure. Hapo pia Kinshasa, Bujumbura na Monusco wamekanusha.

Kwa mujibu wa wakaazi wa Kiliba, vijana wa chama madarakani nchini Burundi, Imbonerakure, waliondoka katika maeneo hayo ya Kiliba mwishoni mwa mwezi wa Mei. Lakini wanaharakati wawili wa mashrika ya kiraia nchini Congo wamethibitisha kwamba waliwahi kufanyiwa vitisho baada ya kutoa taarifa ihusuyo wanajeshi hao wa Burundi katika aridhi ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.