Pata taarifa kuu
KENYA-UHURU-UGAIDI-USALAMA

Maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru

Wakenya leo Ijumaa Desemba 12 wanaadhimisha miaka 51 ya uhuru, waliopata kutoka kwa wakoloni kutoka Uingereza mwaka 1963. 

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kulia) akiwa pamoja na makamu wa rais William Ruto, wakati ambapo Kenya inaadhimisha miaka 51 ya uhuru wake.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta (kulia) akiwa pamoja na makamu wa rais William Ruto, wakati ambapo Kenya inaadhimisha miaka 51 ya uhuru wake. AFP/Simon Maina
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta ataongoza maadhimisho ya leo katika uwanja wa Taifa wa Nyayo jijini Nairobi.

Maadhimisho haya yanakuja wakati huu Kenya ikikabiliwa na changamoto za usalama, kutokana na mashambulizi ya kigaidi kutoka kundi la Al Shabab kutoka mjini Mombasa.

Kenya ilipata uhuru wake, siku kama ya leo baada ya mapambano ya muda mrefu na Waingereza waliokuwa wanatawala nchi yao na kunyakua mashamba yao.

Wakati wa ukoloni, raia wa Kenya hawakuruhisiwa kumiliki ardhi wala kupiga kura.

Uongozi wa kimabavu ulichochea raia wa Kenya kuunda vuguvugu la Mau Mau kupambana na wakoloni hao kati ya mwaka 1952 hadi 1960.

Wakati wa juhudi za kupata uhuru, maelfu ya watu walipoteza maisha wakipigania uhuru wa nchi yao wakiongozwa na kiongozi wa Mau Mau Dedan Kimathi aliyekamatwa katika harakati hizo.

Baada ya harakati hizo, Kenya hatimaye ilipata uhuru wake na kuwa Jamhuri siku kama ya leo na Jomo Kenyatta, kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo.

Kenya inaadhimisha miaka 51 ikikabiliana na changamoto ya kiusalama ambayo serikali ya sasa inayoongzwa na rais Uhuru Keenyatta ikiendelea kupata shinikizo kuimarisha usalama nchini humo.

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka nchini Somalia limekuwa likiishambulia Kenya. Mauaji ya hivi karibuni yaliyotokea mjini Mandera ambapo watu zaidi ya 60 walipigwa risasi, yameendelea kusababisho mdororo wa kiusalama.

Al Shabab inasema inatekeleza mauji hayo kwa sababu jeshi la Kenya liliingia nchini mwao mwaka 2011 ili kupambana nao.

Kikosi cha wanajeshi wa Kenya kikiwasaka wanamgambo wa Al Shabab katika kijiji cha Dobley.
Kikosi cha wanajeshi wa Kenya kikiwasaka wanamgambo wa Al Shabab katika kijiji cha Dobley. RFI/Stéphanie Braquehais

Mbali na changamoto za usalama, Kenya inajivunia kuwa nchi ya kwanza katika eneo la Afrika Mashariki baada ya uhuru wake miaka hamsini iliyopita kupata katiba mpya ambayo imepunguza madaraka ya rais, na kuanzisha mfumo wa serikali za Kaunti ili kuendeleza maendeleo.

Marais ambao wameongoza Kenya tangu Uhuru ni pamoja na Jomo Kenyatta, Daniel Arap Moi, Mwai Kibaki na sasa Uhuru Kenyatta.

Kenya ambayo ni nchi inayoongoza kwa uchumi katika nchi za Afrika Mashariki na ina watu milioni 44.

Wanamgambo wa Al Shabab, ambao wameapa kuendelea na mashambulizi katika ardhi ya Kenya, licha ya nchi ya hiyo kuendelea kukua kiuchumi.
Wanamgambo wa Al Shabab, ambao wameapa kuendelea na mashambulizi katika ardhi ya Kenya, licha ya nchi ya hiyo kuendelea kukua kiuchumi. (Photo : Reuters)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.