Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-Sheria-Haki za binadamu

ICC yampa wiki 1 Fatou Bensouda kuendelea au la na kesi ya Kenyatta

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC imekataa ombi la Mwendeska mashitaka mkuu, Fatou Bensouda, kuahirisha kesi dhidi rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Bensouda amepewa wiki moja kutupilia mbali kesi hiyo au aiarifu Mahakama kwamba amepata ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda.
Mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama hiyo wamekataa pia hoja ya Mwendesha mashitaka Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kutoa ushirikiano.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters

Uamzi huo umekua unasubiriwa kwa hamu na gamu, baada ya rais wa Kenya kujielekeza Hague mwezi Oktoba. Kenyatta alitakiwa kuripoti mbele ya majaji wa Mahakama hiyo ili upande wa mashitaka na upande wa utetezi mbili waisikilizwe, na Mahakama iamuwe iwapo kesi hiyo iendelee au isitishwe.

Mahakama imechukua uamzi huo Jumatano Desemba 3. Awali Fatou Bensouda alikiri mwenyewe kwamba hana ushahidi wa kutosha, lakini aliomba apewe muda ili aendelee kutafuta ushahidi, akibaini kwamba mashahidi aliokua nao waliamua kujiondoa katika kesi hiyo. Bensouda aliituhumu serikali ya Kenya kwamba ilikataa kutoa ushirikiano.

Fatou Bensouda apewa makataa na ICC kuhusu uhuru Kenyatta.
Fatou Bensouda apewa makataa na ICC kuhusu uhuru Kenyatta. EMMANUEL DUNAND / AFP

Bensouda alikusudia kupata ushahidi kutoka upande wa serikali ya Kenya, akiitaka serikali kutoa nyaraka muhimu zinazo muhusu Kenyatta ambazo zingelionyesha kuwa alihusika katika ghazia za baada ya uchaguzi katika mwaka wa 2007 hadi 2008. Hata hivyo Mahakama ilitupilia mbali kwamba serikali ya Kenya ilikataa kutoa ushirikiano.

Itafahamika kwamba watu 1200 waliuawa katika ghasia hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.