Pata taarifa kuu
CAMEROON-NIGERIA-BOKO HARAM--Usalama

Askari 8 wa Cameroon watoweka

Nchini Cameroon hali ya utulivu imerejea katika kambi ya kijeshi ya Achigachia baada ya mapigano yaliotokea Jumapili Desemba 28 dhidi ya kundi la Boko Haram.

Askari wa Cameroon tarehe 17 Juni mwaka 2014, wakizidisha ulinzi kwenye ngome yao katika mji wa mpakani wa Amchide katika mkoa wa kaskazini mwa nchi, mji unakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram.
Askari wa Cameroon tarehe 17 Juni mwaka 2014, wakizidisha ulinzi kwenye ngome yao katika mji wa mpakani wa Amchide katika mkoa wa kaskazini mwa nchi, mji unakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram. Reinnier KAZE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza jeshi la Cameroon limetumia ndege na kuendesha mashambulizi ya anga, baada ya boko Haram kupenya na kuingia katika kambi hiyo ya kijeshi na kuishikilia kwa muda wa masaa kadha. Mapigano yalikua si ya kawaida. Jeshi limetoa idadi ya kwanza ya askari wanane ambao hawajulikani walipo.

Habari hii ni kwa mujibu wa chanzo cha uongozi wa majeshi nchini Cameroon. Chanzo hicho kimebaini kwamba askari hao ambao hawakuonekana wakati wa zoezi la kuhesabu askari lilofanyika Jumatatu Desemba 29 katika kambi ya Achigachia, wanadaiwa na uongozi wa jeshi kuwa waliuawa.

Hata hivyo idadi ya vifo upande wa Boko Haram, haikutangazwa. Huenda Boko Haram wakawa wamepata hasara kubwa, wizara ya ulinzi ya Cameroon imeeleza.

Wizara hiyo imebaini kwamba maelfu ya wapiganaji wa Boko Haram walivamia kambi hiyo ya kijeshi na kuiteka kwa muda wa masaa kadhaa, lakini ndege ilifaulu kuteketeza kambi hiyo, kwa sasa kambi hiyo imebaki tu ni jivu, na hiyo ni moja ya dalili zinazoonyesha kuwa Boko Haram wamepata hasara kubwa, imeendelea kusema wizara ya ulinzi ya Cameroon.

Baada ya kutimuliwa kutoka katika kambi hiyo , wapiganaji wa Boko Haram walikwenda hadi kwenye umbali wa kilomita tano na kambi hiyo, upande wa Nigeria katika kambi moja ya kijeshi ambayo wanashikilia tangu miezi kadhaa iliyopita.

Hali katika uwanja wa mapigano bado inatatanisha. Viongozi mbalimbali walikutana Jumatatu Desemba 29, na vikao hivyo viliendelea hadi jioni.

Kwenye majira ya mchana mkuu wa majeshi pamoja na maafisa wengine katika jeshi waliondoka katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde na kujielekeza katika eneo la vita.

Wakati huo huo gari la jeshi lilishambuliwa kwa bomu lililokua lilitegwa ardhini kwenye barabara inayoelekea Amchidé-Kolofata, katika mkoa wa Kaskazini mwa Cameroon. Shambulio hilo limewaua askari wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.