Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-MAANDAMANO-USALAMA

Burundi: serikali yaonya waandamanaji

Baada ya makabialiano yaliyotikea Ijumaa juma lililopita kati ya polisi na waandamanji dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza, hatimaye serikali ya Burundi imewaonya waandamanaji na wanasiasa wanaoendelea kuchechea maandamano.

Polisi ilitumia mizinga ya maji kwa kuwatawanya waandamanaji jijini Bujumbura Aprili 17 mwaka 2015.
Polisi ilitumia mizinga ya maji kwa kuwatawanya waandamanaji jijini Bujumbura Aprili 17 mwaka 2015. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari serikali ya Burundi kupitia mawaziri wane, ulinzi, usalama, sheria na mambo ya ndani, wameonya wanasiasa wa upinzani ambao wamekua wakiwatolea wito wafuasi wao kuingia mitaani, kwa lengo la kusababisha vurugu, kwa mujibu wa mawaziri hao.

Hayo yanajiri wakati watu 65 wanaendelea kuzuiliwa katika jela kuu la mkoa wa Muramvya, katikati mwa Burundi. Walikamatwa na polisi Ijumaa juma lililopita katika maandamano yaliyoitishwa na vyama vitano vya upinzani vikishirikiana na baadhi ya vigogo wa chama tawala kwa kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza. Ofisi ya mshtaka katika jiji la Bijumbua inawatuhumu kuhusika katika vurugu zenye lengo la kuuangusha utawala uliopp madarani.

Waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana amesema kuwa vikosi vya usalama na utawala watachukua hatua zinazohitajika kwa kuaadhibu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika na waandalizi wa maandamano hayo.

Waziri Edouard Nduwimana amevitaka vyama hivyo vya upinzani kufuatisha utaratibu wa kufanya maandamano, huku akiwaomba viongozi wa vyama hivyo kuwasilisha ombi lao la kufanya maandamano ili waweze kuruhusiwa.

Haata hivyo viongozi wa vyama hivyo vya upinzani wameapa kuendelea na maandamano hayo, huku wakibaini kwamba hawatokubali kutishwa na kauli za viongozi wa serikali.

Viongozi hao wa vyama vya upinzani wamekua wakimlaumu waziri wa mambo ya ndani na pamoja na waziri wa usalama ambao wamekua wakiunga mkono maandamano ya chama tawala cha Cndd-Fdd, bila hata hivyo kuandika barua ya kuomba kufanya maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.