Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA

Burundi : shughuli zakwama mjini kati Bujumbura

Shughuli zimekwama leo Ijumaa mjini kati Bujumbura, nchini Burundi, baada ya vurugu kutokea kufuatia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.

Umati wa watu waliokusanyika nje ya makao makuu ya radio RPA wakisubiri kuachiliwa huru kwa mkurugenzi wa radio hiyo, Bob Rugurika, aliyekua akizuiliwa jela kwa kipindi cha mwezi mmoja mkoani Muramvya katikati mwa Burundi, Februari 18 mwaka 2015.
Umati wa watu waliokusanyika nje ya makao makuu ya radio RPA wakisubiri kuachiliwa huru kwa mkurugenzi wa radio hiyo, Bob Rugurika, aliyekua akizuiliwa jela kwa kipindi cha mwezi mmoja mkoani Muramvya katikati mwa Burundi, Februari 18 mwaka 2015. AFP PHOTO/Esdras NDIKUMANA
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa vyama vitano vya upinzani ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafuasi wenye ushawishi mkubwa kutoka chama tawala cha Cndd-Fdd ambao wanapinga nia ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula watatu katika uchaguzi ujao wa urais wameandamana na wafuasi wao mjini kati Bujumbura wakimtaka rais Pierre Nkurunziza kutogombea muhula watatu, ambao ni kinyume na Katiba ya Burundi pamoja na Mkataba wa amani wa Arusha.

Kama alivyoshuhudiwa mwandishi wa RFI katika maeneo mbalimbali ya mjini kati Bujumbura, polisi ilitumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na magari maalumu dhidi ya vurugu kwa kuwatawanya waandamanaji.

Baadhi ya askari polisi wamekua wamevalia kofia za chuma pamoja na ngao mkononi. Hata hivyo polisi imewakamata baadhi ya waandamanaji na raia wengine ambao walikua wamejielekeza mjini kati kununua chakula na vifaa vingine mahitajio. Askari polisi kadhaa wamejeruhiwa baada ya kurushiwa mawe na waandamanaji.

Awali mashirika ya kiraia yalitishia kuandamana iwapo polisi itawakamata au kuwajeruhi waandamanaji. Wakati huohuo mashirika hayo ya kiraia yametishia kutolea wito raia kuingia mitaani iwapo chama cha Cndd-Fdd kitamtangaza rais Pierre Nkurunziza kuwania katika uchaguzi ujao wa Urais.

Chama cha Cndd-Fdd kinatazamia kumtangaza Jumamosi mwishoni mwa juma hili rais Nkurunziza kuwania muhula watatu.

Itafahamika kwamba Jumanne wiki hii vyama vitano vya upinzani ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafuasi vigogo wa chama tawala cha Cndd-Fdd valiwatolea wito wafuasi wao kuanza kuingia mitaani tangu Jumatao Aprili 15 mwaka 2015.

Lakini wizara ya mambo ya ndani kupitia katibu wake wa kudumu ilipiga marufu maandamano hayo, ikibaini kwamba hayafuatishi sheria.

Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita chama tawala cha Cndd-Fdd kiliandaa maandamano ya kumuunga mkono rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula watatu, bila hata hivyo kubughudhiwa. Na polisi ilitoa ulinzi wa kutosha katika maandamano hayo.

Kila mara upinzani au vyama vya kiraia vinapofanya maandamano, serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani imekua ikipinga maandamno hayo, ikibaini kwamba hayafuatishi sheria, lakini chama tawala kimekua kikirahisishiwa katika maandamano yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.