Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Mapigano-Usalama

Jeshi la Ukraine laendelea kuwatimua waasi

Jeshi la Ukraine linaendelea na mashambulizi yake mashariki mwa Ukraine,katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi, hususana katika jimbo la Donetsk. Awali jeshi la Ukraine lilisindwa kurejesha kwenye himaya yake baadhi ya maeneo yaliyokua yakishikiliwa na waasi. Hivi karibuni jeshi hilo limebaini kwamba limefaulu kurejesha kwenye himaya yake baadhi ya maeneo.

Jeshi la Ukraine lashambulia nyumba walikokua wakiishi viongozi wa waasi , karibu na mji wa Donetsk, masahariki mwa Ukraine.
Jeshi la Ukraine lashambulia nyumba walikokua wakiishi viongozi wa waasi , karibu na mji wa Donetsk, masahariki mwa Ukraine. REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ukraine iliamuru jeshi kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa Ukraine. Baadhi ya maeneo muhimu yanayoshikilwa nawaaasi yalilengwa, tangu ilipoanzishwa operesheni hiyo.

Jeshi la Ukraine kwa saa imekua ikirejesha baadhi ya maeneo, ikiwemo miji muhimu. Jeshi hilo linaendelea kwa sasa na operesheni hiyo katika maeneo ya kaskazini na kusini, na limebaini kwamba linaukurubia mji wa Donetsk.

Hayo yakijiri mapigano yanaripitiwa kwa sasa katika mji wa Gorlivka, ambo ni eneo muhimu kwa waasi, baada ya kutimuliwa katika ngome yao kuu ya Sloviansk. Jeshi la Ukraine limekiri kukiteka kijiji cha Debaltseve. Hapo jumapili, watu 14, wakiwemo watoto waliuawa katika mashambulizi ya roketi aina ya Grad.

Jumatatu wiki hii, jeshi la Ukraine lilfaulu kurejesha kwenye himaya yake eneo muhimu la Donetsk, ilikodunguliwa ndege ya malaysia Airlines. Kwa mujibu wa serikali ya Ukraine, jeshi liliingia katika maeneo ya Chakhtarsk na Torez na kurejesha kwenye himaya yake kijiji cha Savour-Moguyla, ambacho ni eneo muhimu pia kwa waasi, walicho kua wakitumia kwa kuhifadhi na kupata silaha kutoka Urusi.

Baadhi ya mabaki ya ndege ya Malaysia Airlines yamekua yakionekana katika baadhi ya maeneo yanayoshikiliwa na waas.
Baadhi ya mabaki ya ndege ya Malaysia Airlines yamekua yakionekana katika baadhi ya maeneo yanayoshikiliwa na waas. REUTERS/Sergei Karpukhin

Mapema jumanne asubuhi wiki hii, tovuti ya ikulu ya Kiev imetangaza kwamba jeshi la Ukraine likiteka kijiji cha Stepanivka, kusini na eneo ilikodunguliwa ndege ya Malaysia Airlines.

Operesheni hiyo ya kijeshi imezua hisia na lawama kutoka Urusi dhidi ya Ukraine. Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Vitali Tchourkine, ameituhumu Ukraine kukiuka azimio 1266 la Baraza la Usalama la Umoaja wa Mataifa, ambalo limezitaka pande husika katika mapigano nchini Ukraine kusitisha mapigano kwenye eneo ilikodunguliwa ndege ya Malaysia Airlines.

Hapo jumatatu, msemaji wa jeshi ameeleza kwamba jeshi haliendeshi operesheni hiyo kwa lengo la kudhibiti moja kwa moja eneo hilo. Kwa mujibu wa Andrij Lissenko, lengo ni kiuwatimua waasi katika eneo hilo na kulirejesha kwene himaya yake. Mapigano hayo yamepelekea askari polisi kutoka Uholanzi na Australia kushindwa kwa siku ya pili mfululizo kufika kwenye eneo la tukio.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.