Abe alaani kitendo cha utekaji nyara cha IS
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani onyo la kundi la Islamic State kutishia kumuua Kenji Goto, mateka raia wa Japan wanayemshikilia.
Imechapishwa:
Kundi la wapiganaji ewa Dola la Kiislamu limetoa muda wa saa 24 zijazo kwakata vichwa mateka ho iwapo serikali za nchi hizo mbili hatotekeleza masharti lililoyatoa.
Islamic State inasema, Bwana Goto na Rubani kutoka Jordan watauawa kwa kukatwa kichwa ikiwa nchi ya Jordan haitamwachilia huru mwanamke mmoja aliyehukumiwa kifo.
Waziri Mkuu Abe, amesema serikali yake inashirikiana na Jordan kuhakikisha kuwa mateka hao wanaachiliwa huru.
Jumapili iliyopita, Islamic State ilimuua kwa kumkata kichwa mateka mwingine wa Japan Haruna Yukawa.
Awali kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu lilidai serikali ya Japani fidia ya dola milioni 200 kwa ajili ya kuokoa maisha ya raia wake waili lililokua likiwashikilia mateka. Kundi hilo lilitoa masaa 72 kwa serikali ya Japani ili iwe imeshalipa pesa hizo.
Tokyo haikuchelewa kujibu, ikithibitisha kwamba haitashinikizwa wala kutishwa na ugaidi.