Pata taarifa kuu
ISRAEL - USALAMA

Netanyahu aonya kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi ya Iran ni hatari hata kuliko wapiganaji wa Kiislamu wa Islamic State ikiwa wataendelea na mradi wake wa Nyuklia wakati huu majadiliano kuhusu mpango huo yakielekea kwenye tamati.

Benyamin Netanyahu kwenye jukwa la Umoja wa Mataifa UN Septemba  29, 2014.
Benyamin Netanyahu kwenye jukwa la Umoja wa Mataifa UN Septemba 29, 2014. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataufa jijini New York, Netanyahu amesema dunia inapoendelea kupambana na wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq, Iran nayo lazima izuiliwe kuendelea na mradi wake ambao anasema unatengeza silaha za maangamizi.

Netanyahu amesema kushindi Islamic State na kuiacha iran kuendelea na mradi wa nyuklia ni kama kushinda mapigano lakini kupoteza vita, na kuongeza kuwa ni kitisho kikubwa sana kwetu sote.

Netanyahu ameemdelea kuwa uwezo wa Nyuklia wa Iran lazima ukomeshwe, kwa sababu jamhuri ya Kiislam ni utawala hatari sana duniani.

Waziri mkuu huyo amesema Iran inauhadaa ulimwengu wakati huu nba kutaka kufikia muafaka katika mazungumzo na nchi zenye nguvu duniani, wakati ambapo inaeleweka wazi kwamba lengo hasa la Utawala wa Iran ni kutengeneza bomu la nyuklia.

Mazungumzo kati ya Iran na nchi sita zenye nguvu, yanaelekea kufikia kikomo Novemba 24 mwaka huu ambapo makubaliano yanataraji kufikiwa juu ya kuondowa shaka kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran, huku jumuiya ya kimataifa ikiondowa vikwazo dhiri ya utawala wa Teheran.

Urutubishwaji wa madini ya Uranium imekuwa swala tete katika mazungumzo, Urutubishwaji wa Uranium kwa kiwango cha chini unapelekea viwanda kupata nguvu ya umeme, lakini urutubishwaji kwa kiwango cha juu unaweza kusababisha utengenezwaji wa bomu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.