Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-IS-KOBANE-Ushirikiano-Mapigano-Usalama

Jeshi la Marekani lazidisha mashambulizi Kobane

Ndege za kivita za Marekani zimeendeleza mashambulizi ya angaa katika mji wa Kobane nchini Syria dhidi ya waasi wa Dola la Kiislam.

Mashambilizi ya anga katika mji wa Kobane, Oktoba 14 mwaka 2014.
Mashambilizi ya anga katika mji wa Kobane, Oktoba 14 mwaka 2014. RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mashambulizi hayo yakiendelea, Makamanda wa wapiganaji wa Kikurdi wanaopambana na Islamic State ardhini nao wanaomba silaha zaidi kuendeleza mapambano hayo.

Imeripotiwa kuwa, wapiganaji wa Dola la kiislam wameanza kuelemewa katika mji huo karibu na nchi ya Uturuki, lakini Marekani imesema vita hivyo vitachukua muda mrefu.

Hata kama Marekani ilitangaza hivi karibuni kwamba lengo lake ni kuwatimua wapiganaji wa Dola la Kiislam katika ardhi ya Iraq, kwa muda wa siku kadhaa mashambulizi yake yamekua yakilenga maeneo ya kijeshi ya Syria, hasa pembezuni mwa mji wa Kobane, kwenye mpaka na Uturuki.

Zaidi ya mashambulizi 30 yametekelezwa na jeshi la Marekani tangu Jumatano hadi jana Alhamisi na kusababisha vifo vingi upande wa wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Wapiganaji wa Kikurdi wa Syria wameonekana kujidhatiti, na kuamua kurudi kwenye uwanja wa mapigano kutokana na mashambulizi yanayoendeshwa na Marekani na washirika wake.

Hata hivo wapiganaji wa kikurdi wanaendelea kuuawa katika mapigano hayo, licha ya kuendelea kusaidiwa na Marekani na washirika wake. Wapiganaji wanaouawa katika uwanja wa mapigano huzikwa Uturuki upande wa pili wa mpaka.

Mazishi ya wapiganaji wa Kikurdi waliouawa katika mji wa Kobane, Oktoba 14 mwaka 2014.
Mazishi ya wapiganaji wa Kikurdi waliouawa katika mji wa Kobane, Oktoba 14 mwaka 2014. REUTERS/Umit Bektas

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.