Pata taarifa kuu
URUSI-SOKA

Urusi: idadi ya wachezaji wa kigeni katika vilabu imo mbioni kupunguzwa

Serikali ya Urusi iko mbioni kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni wanaochezea vilabu mbalimbali nchini Urusi, ili kuwapa nafasi ya kujiendeleza wachezaji wa Urusi, waziri wa michezo wa Urusi, Vitaly Mutko, ametangaza.

mchezaji wa timu ya taifa ya Urusi, Zyryanov akiwa mbele ya lango la timu ya taifa ya Swedwen.
mchezaji wa timu ya taifa ya Urusi, Zyryanov akiwa mbele ya lango la timu ya taifa ya Swedwen. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo ameeleza kwamba sheria kuhusu kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni katika vilabu vya Urusi imekua ikiandaliwa na huenda ikaanza kutekelezwa hivi karibuni.

"Nous souhaitons que les sportifs russes jouent un rôle de premier plan dans les clubs du pays", a indiqué Vitaly Mutko à l'agence de presse ITAR-TASS.
“ Tunahitaji wachezaji, raia wa Urusi wapewe na fasi ya kwanza katika kuchezea vilabu vya nyumbani”, Vitaly Mutko ameambia shirika la habari la Urusi ITAR-TASS.

Wakati sheria hiyo itaanza kutekelezwa kila klabu itatakiwa kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi sita. Vilabu vya Hockey, volley na Basket vitakua na wachezaji wa kigeni watatu pekee.

Mwezi Mei, kocha wa timu ya taifa ya soka ya Urusi, Fabio Cpello, ambaye ni raia wa Italia, alibaini kwamba wingi wa wachezaji wa kigeni katika vilabu vya soka vya Urusi vitaathiri timu ya taifa ya soka.

Kwa mujibu wa waziri wa michezo, sheria hiyo mpya ambayo itaanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka ujao itapelekea timu ya taifa ya soka inafanya vizuri katika michuano ya kimataifa, hasa michuano ya Kombe la dunia ya mwaka 2018, ambayo Urusi itakua mwenyeji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.