Pata taarifa kuu
SENEGAL-Siasa

Abdoulaye Wade atarajiwa kuwasili Senegal

Rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade anatarajiwa kuwasili hii leo mijini Dakar baada ya ndege iliomsafirisha kuzuiliwa kutua mjini humo jumatano iliyopita. Abdulaye Wade ambaye ameamua kurejea nchini mwake baada ya miaka miwili ya uhamisho nchini Ufaransa, huku kesi ya mwanae Karim Wade ikipamba moto.

Abdoulaye Wade rais wa zamani wa Senegal akitarajiwa kuwasili mjini Dakar.
Abdoulaye Wade rais wa zamani wa Senegal akitarajiwa kuwasili mjini Dakar. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Jumatano asubuhi ndege iliomsafirisha ilitua Casablanca nchini Morocco na kumshushia lawama rais wa Senegal Macky Sall kumzuia kuingia nchini humo.

Wade anarejea leo nchini Senegal kumuunga mkono mwanae Karim Wade anaeziwiliwa, baada ya kukosekana nchini humo kwa muda wa miaka miwili.

Vijana wafuasi wa Abdoulaye Wade wakisheherekea jumatano aprili 23 kurejea kwa rais huyo wa zamani Sénégal.
Vijana wafuasi wa Abdoulaye Wade wakisheherekea jumatano aprili 23 kurejea kwa rais huyo wa zamani Sénégal. FP PHOTO/SEYLLOU

Rais huyo wa zamani wa Senegal alitarajiwa kuwasili mjini Dakar tangu jumatano akitokea mjini Paris nchini Ufaransa, lakini ndege iliyokua inamsafirisha ilitua mjini Cassablanca na kuendelea kusalia kwenye uwanja wa ndege wa mjini Cassablanca kwa kusubiri idhini ya viongozi wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa mjini Dakar, huku wafuasi wake na serikali wakitupiana lawama kuhusu kucheleweshwa kwa ndege hio.

“Nilielewa tangu kitambo kwamba Macky Sall hataki nirejeye”, amesema Wade, akilani mbinu zinazotumiwa na utawala wa Macky Sall wa kuzuia ili asiendeleyi na safari yake hadi mjini Dakar.

Abdulaye Wade , mwenye umri wa miaka 87, amesema kwamba alisubiri kwa muda wa saa zaidi ya tatu ili apewe idhini ya kuendelea na safari bila mafaanikio.

Ndege ya kibinafsi iliyokodiwa na Wade iliondoka mjini Paris jumatano na ingelipaswa kutua mjini Dakar siku hiohio, ambapo mkutano mkuu wa wafuasi wa Wade ulikua unasubiriwa kufanyika baada tu ya kuwasili kwake mjini Dakar.

Hoteli Hyatt Regency ya mjini Casablanca, nchini Morocco, ambako amefikia Abdoulaye Wade.
Hoteli Hyatt Regency ya mjini Casablanca, nchini Morocco, ambako amefikia Abdoulaye Wade. AFP/Stringer

Abdulaye Wade ameamua kurejea nchini ili kuja kumuunga mkono mwanae Karim Wade, ambae anaziwiliwa kwa muda tangu mwaka moja uliyopita.

Korti maalumu ya nchini Senegal imeamua kumsikiliza Karim Wade kuanzia mwezi wa juni kuhusu tuhumu za kujitajirisha kinyume cha sheria zinazo mkabili kwa kipindi cha miaka 12 cha uongozi wa baba yake, ambae alikua mshauri wake wa karibu, na baadae waziri mwenye madaraka makubwa.

Karim Wade, mwenye umri wa miaka 45, anakanusha tuhuma dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.