Pata taarifa kuu
Senegal-Uchaguzi

Makcy Sall kuapishwa April 3 jijini Dakar

Shughuli za kupeana madaraka baina ya Abdoulaye Wade mwenye umri wa miaka 85 madarakani tangu miaka 12 iliopita, na rais mteule Macky Sall mwenye umri wa miaka 50, zimepangwa kufanyika April 2, zitazofuatiwa April 3 na sherehe za kula kiapo. April 4 rais huyo mteule ataongoza sherehe za Uhuru wa nchi hiyo. Kuanzia April 7, orodha ya majina ya wagombea uchaguzi wa bunge unaotarajiwa mwezi Juni yanatakiwa kuwa tayari kuwakilishwa.

Kundi la wafuasi wa  Macky Sall, rais mteule wakisherehekea ushindi
Kundi la wafuasi wa Macky Sall, rais mteule wakisherehekea ushindi © Reuters/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo mteule ameanza tayari shughuli za kuwapokea mabalazi na wajumbe wa tume uangalizi wa uchaguzi kwenye Hoteli moja jijini Dakar. Amekutana pia na wajumbe wa chama chake ili kuwatolea shukrani kwa kazi kubwa walioifanya ilipelekea kuupata ushindi.Pongezi zimekuwa zikitolewa kutoka nje na ndani ya nchi hiyo.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni uundwaji wa serikali yake, ambapo tayari ameanza harakati za kutafuta wajumbe watao shirikisha katika serikali hiyo, bila shaka ni kutoka pande mbalimbali wakiwemo wajumbe wa vyama vilivyo muunga mkono kufikia kwenye hatuwa hiyo.

Wananchi wa Senegal wameutupilia mbali utawala wa Abdoulaye Wade kutokana na jeuri yake na ubabe, na ubadhirifu wa mali ya Umma, imesema duru kutoka kwa watu wa karibu na rais mteule.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.