Pata taarifa kuu
NIGERIA-Maandamano

Maandamano ya wanawake yafanyika nchini Nigeria

Familia za wasichana waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram, nchini Nigeria zinapanga kuandamana leo mjini Abuja katika kile wanachokisema kama kuishinikiza serikali kuhakikisha watoto wao wanarejeshwa wakiwa hai.

Wazazi wa wasichana waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram, aprili 14 avril.
Wazazi wa wasichana waliyotekwa nyara na kundi la Boko Haram, aprili 14 avril. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika huku kukiwa na taarifa kwamba wasichana hao waliotekwa nyara majuma mawili yaliyopita, walionekana wakivushwa mpaka kati ya Nigeria na mataifa jirani kama Cameroon na Chad.

Zaidi ya wasichana mia mbili wakiwa ni wanafunzi katika shule ya mabweni iliyoko mjini Chibok katika jimbo la Borno kaskazini mwa Nigeria walitekwa nyara na kundi la Boko Haram aprili 14, huku baadhi ya wasichana wakilazimishwa kuolewa na wapiganaji hao.

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi la Boko Haram. AFP PHOTO/YOUTUBE

Kwa mujibu wa wasichana waliyofaulu kutoroka watekaji nyara hao, wamebaini kwamba walipotekwa nyara, walipelekwa hadi katika msitu wa Sambisa, mashariki mwa jimbo la Borno, ambako kundi la Boko Haram limejenga kambi.

Jeshi la Nigeria lilitangaza ijuma iliyopita kwamba liliwaua wanamgambo 40 wa kundi la Boko Haram karibu na msitu wa Sambisa, wakati wa operesheni ya kuwatafuta wasichana hao waliyotekwa nyara, bila hata hivo ktoa taarifa zaidi.

Kundi la Boko Haram, limekua likilenga sehemu wanakokusanyika watu wengi, hasa shule zinazopatikana kaskazini mwa Nigeria, ambako watu wengi wanaoishi eneo hilo ni kutoka jamii ya waislam

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.