Pata taarifa kuu
MISRI

Mahakama nchini Misri kutoa hukumu dhidi ya Wanahabari wa Al- Jazeera

Mahakama jijini Cairo nchini Misri inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya wanahabari watatu wa kituo cha Al-jazeera ambao wamekuwa wakizuiliwa tangu mwezi Desemba mwaka uliopita.

Wanahabari watatu wa Al Jazeera Mohammed Fahmy , Baher Mohamed na Peter Greste
Wanahabari watatu wa Al Jazeera Mohammed Fahmy , Baher Mohamed na Peter Greste
Matangazo ya kibiashara

Wanahabari hao Peter Greste, Mohammed Fahmy na Baher Mohamed wanatuhumiwa kushirikiana na kundi lililoharamishwa la Muslim Brotherhood na kusambaza habari za uongo, tuhma ambazo wanahabari hao wamekanusha.

Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu na Jumuiya ya Kimataifa imekuwa ikiishinikiza serikali ya Misri kuwaachilia huru Wanahabari hao ambao wamekuwa wakifikishwa Mahakamani mara kwa mara.

Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott amekuwa miongoni mwa viongozi wa dunia ambao wameendelea kuishinikiza serikali ya Misri kuwaachilia wanahabari hao hasa Peter Grester ambaye ni raia wa Australia.

Vongozi wa Mashtaka wamewaomba Majaji kuwafunga jela wanahabari hao kati ya miaka 15 na 25 kwa kile wanachosema kuwa ushahidi wao umedhihirisha wazi kuwa walishirikiana na kundi la Muslim Brotherhood na kusambaza habari za uongo.

Pamoja na wanahabari hao, Mahakama hiyo pia imekuwa ikisikiliza kesi dhidi ya watu wengine 20 wanaotuhumiwa kuhusika na kundi hilo.

Mapema mwezi huu, Mahakama jijini Misri ilimwachilia huru Mwanahabari mwingine wa Al-Jazeera,  Abdullah Elshamy kwa sababu za kiafya.

Elshamy alikuwa anazuiliwa bila ya kufunguliwa Mashtaka na aligoma kula kuanzia mapema mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.