Pata taarifa kuu
UFARANSA-Vita vya kwanza vya dunia-Siasa

Ufaransa : maadhimisho ya miaka 100 tangu vita vya kwanza vya dunia vimalizike

Maadhimisho ya sherehe za kitaifa za tarehe 14 mwezi Julai nchini Ufaransa yamefanyika jumatatu wiki hii ambako viongozi wa nchi zisizopungua 80 wamealikwa kuhudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika sambamba na kumbukumbu ya miaka mia tangu vita vya kwanza vya dunia vimalizike.

Rais wa Ufaransa, François Hollande.
Rais wa Ufaransa, François Hollande. Capture écran France 2
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa imealika katika sherehe hizo mataifa mbalimbali yakiwemo mataifa ishirini ya kiafrika yaliyoshiriki kwa upande wake katika vita vya dunia. Utawala wa kifalme wa Ufaransa wakati huo ulitumia maeneo yaliyokua chini ya milki yake katika vita hivyo.

Karibu wafrika milioni moja na nusu walishiki katika vita vya kwanza vya dunia. Takriban watu 200.000 kutoka mataiifa ya magharibi mwa Afrika na wengine 270.000 kutoka mataifa ya kaskazini mwa Afrika ni miongoni mwa walioshiriki vita hivyo upande wa Ufaransa. Sehemu ya watu hao waliingizwa katika jeshi la Ufaransa katika mwaka 1914. Na wengine walijiunga kwa hiyari yao kwa sababu mbalimbali, hususan ushawishi, na kadhalika.

Hata hivyo kuna watu waliolazimishwa kujiunga na jeshi la Ufaransa kwa kushirika vita vya kwanza vya dunia, baadhi waliyahama makaazi yao na kukimbilia misituni wakihofiya usalama wao, na wengine walijua wakikataa kushiriki vita vya kwanza vya dunia.

Mapigano ya kwanza yaliwagharimu maisha watu waliyoshiriki vita hivyo kutokana na magonjwa mbalimbali na wengine kutokana na mafunzo mabovu.

Gwaride la wanajeshi wa Ufaransa mbele ya ikulu "Champs Elysées", mjini Paris, wakati wa siku kuu ya kitaifa.
Gwaride la wanajeshi wa Ufaransa mbele ya ikulu "Champs Elysées", mjini Paris, wakati wa siku kuu ya kitaifa. REUTERS/Christian Hartmann

Katika sherehe za maadhimisho hayo, wanajeshi wa Ufaransa wameonyesha ujuzi wao, huku vifaru, magari ya kijeshi na zana mbalimbali za kijeshi vikionyeshwa katika gwaride ambalo lilmeshuhudiwa na raia wengi.

Katika hotuba yake rais Hollande amesema Ufaransa haiegemeyi upande wowote katika vita vinavyoendeleza kati ya Israeli na Palestina na kukumbusha kwamba hakuna sababu yoyote itayoweza kupelekea Ufaransa inaegemea moja ya Pande hizo. Rais Hollande amesema hayo kufuatia maandamano yanayoshuhudiwa hapa na pale ya kuunga mkono wapalestina  na mji wa Gaza dhidi ya mashambulizi ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.