Pata taarifa kuu
IBYA-Mapigano-Usalama

Libya : Ghala la lita milioni 6 ya mafuta lawaka moto

Ghala kubwa la mafuta linawaka moto karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli, ambao umeshindikana kuzimwa. Ajali hiyo imesababishwa na bomu liliyorushwa kwenye ghala hilo na kusababisha tishio kubwa la kuteketea kwa mji wa tripoli, ambao kwa sasa raia wa kigeni wameukimbia kutokana na mapigano yanayoendelea.

Ghala la mafuta lashambuliwa kwa bomu.
Ghala la mafuta lashambuliwa kwa bomu. Reuters/Thaier al-Sudani
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Libya wamewataka raia wake wanaoishi karibu na ghala hilo kuondoka haraka iwezekanavyo kwa kuhofia kulipuka ghala nyingine na kusababisha moto kusambaa eneo nzima.

Serikali ya Libya imetaka msaada kwa mataifa jirani, ambayo yalitangaza hivi karibuni kwamba yanajianda kutuma ndege.

Ghala hilo ambalo linapatikana kwenye barabara inayoelekea uwanja wa ndege, kunako ripotiwa mapigano kati ya jeshi na makundi ya waasi, linawaka moto tangu jana jumapili na lina lita milioni 6 za mafuta. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 97 na wengine 400 kujeruhiwa, kwa mujibu wa idadi ya hivi karibuni iliyotolewa na serikali.

Licha ya siku kuu ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, milipuko imekua ikisikika hadi leo mchana.

Kwa mujibu wa mpiga picha wa shrika la habari la Ufaransa AFP, mabomu aina ya Grag yamerushwa mchana wa jumatatu wiki hii na kuanguka karibu na ghala linalowaka moto, huku moshi mkubwa ukitanda eneo nzima, kwenye umbali wa kilomita 12 na mji wa Tripoli.

Kumekua na hofu kwamba huenda moto huo ukasambaa baada ya ghala za gezi kushambuliwa kwa moto huo unaoendelea kushika kasi.

Kiwanda cha kusafisha mafuta na gesi kikiwa hatarini ya kushambuliwa kwa moto mjini Tirpoli.
Kiwanda cha kusafisha mafuta na gesi kikiwa hatarini ya kushambuliwa kwa moto mjini Tirpoli. ENI

Libya ni taifa tajiri kwa mafuta, lakini kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa mafuta baada ya vituo vingi vya mafuta kusitisha shughuli ya kuuza mafuta kutoka na kudorora kwa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.