Pata taarifa kuu
BURUNDI-AMNESTY INERNATIONAL-Siasa-Usalama

Burundi : chama tawala na utawala wa Bujumbura vyanyooshewa kidole

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International, linakinyooshea kidole cha lawama chama tawala nchini Burundi Cndd-Fdd kwa kuendesha kampeni ya vitisho dhidi ya vyama vya upinzani, wakati taifa hilo likijiandalia uchaguzi mkuu hapo mwakani.

Amnesty International yanyooshea kidole chama tawala Cndd-Fdd na serikali ya Bujumbura kwa vitisho dhidi ya upinzani na mashirika ya kiraia.
Amnesty International yanyooshea kidole chama tawala Cndd-Fdd na serikali ya Bujumbura kwa vitisho dhidi ya upinzani na mashirika ya kiraia. AFP / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyotolewa na shirika hilo, Amnesty international imesema chama tawala Cndd-Fdd kimekua kikwazo kwa kuendeleza demokrasia nchini Burundi, huku akituhumu utawala kuminya uhuru wa kutoa maoni na kufanyika kwa mikutano vya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia.

“Vitisho vinavyoendeshwa na serikali dhidi ya uhuru wa kutoa maoni na kuminywa kwa mikutano ya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia nvina athari kubwa katika suala nzima la haki za binadamu, wakati taifa hilo likijiandalia uchaguzi mkuu hapo mwakani”, Tom Gibson, ambaye ni mtafiti wa Amnesty International kuhusu Burundi, amebaini.

Jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa , wanatiwa hofu na hali ya kisiasa na usalama inayojiri wakati huu nchini Burundi, hususan kuongezeka kwa machafuku yenye misingi ya kisiasa na kuminywa kwa uhuru. Burundi ni moja ya nchi masikini duniani, ambayo ilitoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2006, vita ambavyo vilidumu miaka 13.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. AFP/Pierre Andrieu

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, anaonekana kutosikia wito taasisi na mataifa mbalimbali ya kumtaka kutogombea muhula wa tatu, licha ya kuwa upinzani unasema kwamba katiba ya taifa hilo haimruhusu kugombea muhula wa tatu.

Amnesty inatiwa hofu na kuongezeka kwa machafuko yenye misingi ya kisiasa, ambayo yanaendeshwa na baadhi ya vijana wa chama tawala Cndd-Fdd “imbonerakure”. Umoja wa Mataifa na mabaolizi mbalimbali wanaendelea kunyooshea kidole “Imbonerakure” kuhusika na machafuko yanayoendelea nchini Burundi, limeongeza Amnesty.

Tom Gibson, amesema vijana hao wa chama tawala “Imbonerakure” wamekua wakishirikiana na baadhi ya asikari polisi kwa kutekeleza maovu mbalimbali ambayo ni kinyume na haki za binadamu, bila hata hivo kuchukuliwa hatua kali.
Afisa mmoja kwenye Umoja wa Mataifa amebaini kwamba vijana hao “Imbonerakure wanakadiriwa kufikia 20.000 nchini Burundi.

Barua ya siri ya Umoja wa Mataifa, iliyosomwa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari vya Burundi, inabaini kwamba utawala wa Bujumbura umekua ukiwapa silaha vijana hao wa chama tawala cha Cndd-Fdd “Imbonerakure”, lakini serikali ilikanusha tuhuma hizo dhidi yake.

Mwezi Machi, vyombo vya sheria nchini Burundi viliwahukulu wafuasi 21 wa chama cha upinzani cha Msd kifungu cha maisha jela na wegine 24 miaka 5 hadi 10 jela, wakituhumiwa kuanzisha kundi lenye silaha dhidi ya utawala, baada ya makabiliano na polis, ambayo iliwakatalia kufanya mkutano.

Alexis Sinduhije, kiongozi wa chama cha upinzani MSD, ambaye kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi.
Alexis Sinduhije, kiongozi wa chama cha upinzani MSD, ambaye kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi. AFP PHOTO/Esdras Ndikumana

Pierre-Claver Mbonimpa, akiwa mahakamani na wanasheria wake.
Pierre-Claver Mbonimpa, akiwa mahakamani na wanasheria wake. RFI/Esdras Ndikumana

Hayo yakijiri mwanaharakati wa haki za binadamu na za wafungwa, Pierre-Claver Mbonimpa amesalia jela tangu mwezi Mei, akituhumiwa kujaribu kuhatarisha usalama wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.