Pata taarifa kuu
LIBERIA-EBOLA-Afya-Usalama

Liberia : kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Ebola chashambuliwa

Hali ya sintofahamu imeendelea kutanda kwenye mji mkuu wa Liberia, Monrovia, baada ya wagonjwa kumi na saba wa Ebola waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye kituo kimoja kukimbia baada ya kituo hicho kuvamiwa na kundi la vijana.

Wanajeshi wa Liberia wakikagua wakaazi wa jimbo la Bomi, kulikotokea shambulio dhidi ya kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Ebola.
Wanajeshi wa Liberia wakikagua wakaazi wa jimbo la Bomi, kulikotokea shambulio dhidi ya kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Ebola. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Uvamizi kwenye kituo hicho kunaelezwa kurudisha nyuma juhudi za Serikali kukabiliana na maradhi haya kwakuwa mpaka sasa haujulikani wagonjwa hao walipokimbilia na kuongeza hofu kuwa huenda wakawaambukiza raia zaidi.

Hapo jana kundi la vijana walivamia kituo cha wagonjwa wa Ebola mjini Monrovia katika kile wanachodai ni kupinga hatua ya wizara ya afya nchini humo kuendelea kuwaleta wagonjwa zaidi kwenye mji huo wakihofia kuambukizwa.

“Wameingia baada ya kuvunja mlango, na kuuanza kupora vifaa vilivyokua katika vyumba kulikokua kumelazwa wagonjwa. Wagonjwa wote wametimka”, amethibitsha Rebecca Wesseh, shuhuda wa tukio hilo lilitokea usiku wa jumamosi kuamkia jumapili.

Kauli hiyo imethibitishwa na wakaazi wa eneo hilo pamoja na katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini Liberia, George Williams.

Kwa mujibu wa Williams, wagonwa 29 wa Ebola walilazwa katika kituo cha afya, ambako wamekua wakipewa huduma za mwanzo kabla ya kuhamishiwa katika hospitali. Wagonjwa wote hao walikutwa na Homa ya Ebola baada ya kufanyiwa vipimo”, amesema Rebecca Williams.

Williams amesema miongoni mwa wagonjwa hao 29, 17 walitimka wakati waliposhambuliwa na vijana hao. Tisa walifariki siku nne zilizopita, na watatu waliondolewa kwa nguvu jumamosi na wazazi wao, na kupelekwa sehemu isiyojulikana, ameongeza Williams.

Mpaka sasa watu elfu 1 mia moja na 45 wameripotiwa kufa kutokana na maradhi ya virusi vya Ebola.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.