Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIERRA LEONE-NIGERIA-Ebola-Afya

Hali ya hatari yatangazwa katika mataifa ya Afrika magharibi

Nchi za Afrika magharibi zimetangaza hali ya hatari kwa kuzidiwa na idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa Ebola ambapo watu wapatao elfu moja sasa wanaripotiwa kufariki kwa maambukizi ya virusi vya Ebola.

Hali ya hatari yatangazwakatika mataifa ya Liberia, Sierra Leone na Nigeria kufuatia kuongezeka kwa vifo kutokana virusi vya Ebola.
Hali ya hatari yatangazwakatika mataifa ya Liberia, Sierra Leone na Nigeria kufuatia kuongezeka kwa vifo kutokana virusi vya Ebola. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo imetangazwa wakati bunge la nchi ya Liberia limekutana kwa dharura kupitisha sheria ya kuweka vizuwizi vya barabarani na kikomo cha usafiri kwa watu wanaoelekea mji mkuu wa Monrovia nchini humo na kuridhia siku 90 ya hali ya hatari.

Aidha, miji miwili mashariki mwa nchi ya Sierra Leone, Kailahun na Kenema, imewekwa chini ya hali ya tahadhari kufwatia kauli ya msemaji wa serikali siku ya Alhamis kuamuru shughuli za vilabu vya usiku na sehemu za burudani na starehe kufungwa.

Mashirika ya kihisani yakihamasisha raia namna ya kupambana dhidi ya virusi vya Ebola nchini Liberia,
Mashirika ya kihisani yakihamasisha raia namna ya kupambana dhidi ya virusi vya Ebola nchini Liberia, REUTERS/Samaritan's Purse

Madaktari wa sekta ya umma nchini Nigeria kwa upande wao wamesitisha mgomo wao wa mwezi mmoja kwa hofu ya ongezeko la maambukizi katika nchi ambayo ni ya kwanza barani Afrika kwa idadi ya wakazi wake na ambapo vifo vya watu wawili na maambukizi ya watu watano vimeripotiwa mjini Lagos.

Daktari bingwa kutoka Marekani, Kent Brantlyalisafirishwa Marekani baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola Katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Daktari bingwa kutoka Marekani, Kent Brantlyalisafirishwa Marekani baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola Katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia. REUTERS/Samaritan's Purse/Handout via Reuters

Wakati hayo yakijiri, Shirika la Afya duniani WHO linatarajiwa ijumaa wiki hii kujadili ikiwa litatangaza hali ya "hatari ya afya kimataifa" katika mkutano wake wa dharura mjini Geneva- Uswisi, pamoja na hatua mpya ikiwa ni pamoja na vikwazo vya kusafiri kimataifa, hasa baada ya serikali ya Uhispania kutuma helikopta ya kijeshi kumrejesha nchini humo daktari Juliana Bonoha Bohe ambaye alifanya kazi katika hospitali moja mjini Monrovia, baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.