Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: Hali ya taharuki imetanda katika mji wa Maiduguri

Marekani imesema inatiwa wasiwasi na kuongezeka kwa mashambulizi ya Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wanajeshi wa Nigeria wakijiandaa kupiga doria usiku katika msitu wa Sambisa, ambao unatawaliwa kwa sehemu kubwa na Boko Haram (Aprili mwaka 2014).
Wanajeshi wa Nigeria wakijiandaa kupiga doria usiku katika msitu wa Sambisa, ambao unatawaliwa kwa sehemu kubwa na Boko Haram (Aprili mwaka 2014). Ben Shemang / RFI
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Nigeria wanaendelea kuthibitisha kwamba bado wana mamlaka kamili katika mji wa Bama, mji wa pili wa jimbo la Borno, kwenye umbali wa kilomita 70 na mji wa Maiduguri. Lakini kwa mujibu wa duru za kuaminika jeshi la Nigeria liliondoka kwenye eneo hilo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Nigeria, Chris Olukolade, amesema kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba eneo la kaskazini mwa Nigeria liko liko chini ya himaya ya jeshi. Msemaji huyo wa wizara ya ulinzi amebaini kwamba jeshi halikuondoka katika mji wa Bama, madai ambayo yanakanushwa na mashahidi pamoja na baadhi ya wanasiasa nchini Nigeria.

Hata hivo idadi ya raia wanayoyakimbia mapigano ambao wanaorodheshwa na Umoja wa Mataifa imeendelea kuongezeka. “ Hatuko katika hatua nzuri ya kujisifu”, amesema naibu waziri wa Marekani anaehusika na masuala ya Afrika, Linda Thomas Greenfield. Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa Marekani inatiwa hofu ya kushambuliwa kwa mji wa Miduguri, baada ya mji wa Bama kuthibitiwa na wapiganaji wa Boko Haram

Katika mkutano uliyozishirikisha nchi ya marekani na Nigeria mjini Abuja, Linda Thomas Greenfield, alitihibitisha kwamba serikali ya Obama imejiandaa kuboresha usalama kwenye mipaka ya jimbo la Borno, huku akibaini kwamba wapiganaji wa Boko Haram wamekua wakijipenyeza na kuhatarisha usalama nchini Nigeria kupitia mzunguuko wa watu kwenye mipaka ya taifa hilo na mataifa jirani ya Cameron, Niger na Chad.

Thomas Greenfield anatazamiwa kuongelea suala hilo atakapo kutana kwa mazungumzo na viongozi wa Cameron jumamosi wiki hii mjini Yaoundé.

Hofu ya mji wa Maiduguri kushambuliwa imepelekea viogozi wa jimbo la Borno kuchukua hatua ya raia kutotembea usiku, huku jeshi na makundi ya watu wanaojihami dhdi ya Boko Haram wakipiga doria usiku na mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.