Pata taarifa kuu
AU-BOKO HARAM-AQMI-AL SHABAB-Usalama

Umoja wa Afrika unatiwa wasiwasi na kuongezeka kwa makundi ya wapiganaji wa kiislam

Mkutano wa Umoja wa Afrika AU umepanga kufanyika jumanne wiki hii jijini Nairobi nchini Kenya kujadili kuhusu kitisho cha makundi ya kigaidi ya kijihadi, mbinu za ya kukabiliana nayo katika kubadilishana taarifa.

Uharibifu unaoendelea kutekelezwa na Boko Haram nchini Nigeria na mataifa jirani.
Uharibifu unaoendelea kutekelezwa na Boko Haram nchini Nigeria na mataifa jirani. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wanaona kwamba makundi ya kigaidi barani Afrika yanaweza kukopi kundi la Islamc State nchini Iraq na Syria licha ya kwamba hawana mahusiano yoyote.

Kundi la Al Shabab nchini Somalia na Kenya, Aqmi nchini Mali na katika ukanda wa Sahel, Boko Haram nchini Nigeria, makundi yota hayo yamekuwa yakidai mafungamano na kundi la Alqaeda na yameteka maeneo kadhaa barani Afrika.

Mbali na hayo viongozi wa Umoja wa Afrika watajadili pia kuhusu umaskini unaendelea kulikumba bara la Afrika pamoja na swala la rushwa ambalo limesalia kwenye miradi katika baadbhi ya mataifa bila hato hivyo kutekelezwa.

Makundi hayo ya wapiganaji wa kiislam yameendelea kujidhatiti katika badhi ya matiafa barani Afrika. Kundi la Ashabab limekua likiendelea na harakati zake katika nchi za Somalia na Kenya, Aqmi nchini Mali na katika jangwa la kusini mwa Sahara, huku Boko Haram ikiendelea na harakati zake katika mataifa ya Nigeria na Cameroon.

Makaundi hayo yameshika mizizi katika bara la Afrika yamekua yakikiri kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la Al Qaeda.

“Muda umewadia kwa mataiafa ya kiafrika kushirikiana kwa pamoja kwa kupeana taarifa ili kutazama namna ya kukabiliana na makundi hayo ambayo yamekua ni tishiyo kwa bara la Afrika”, mkuu wa ujasusi wa Kenya, Chris Mburu, ameambia vyombo vya habari, baada ya mkutano uliyowajumuisha mwioshoni mwa juma wakuu wa ujasusi wa mataifa ya Afrika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.