Pata taarifa kuu
SADC-FDLR-RWANDA-Usalama

SADC yatoa onyo dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR

Jumuiya ya Maendeleo ya kiuchumi kusini mwa bara la Afrika (SADC) imewataka waasi wa Kihutu wa Rwanda waishio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuondoka katika maeneo walioko, la sivyo hatua za kijeshi zitachukuliwa dhidi yao.

Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani).
Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana siku ya Jumatatu mjini Pretoria nchini Afrika Kusini, viongozi hao wameahidi kuwasilishia ujumbe kwa waasi wa FDLR ambao utakuwa wa wazi na kwa nguvu, ambao ni kuwaonya kuwa hatua za kijeshi zitachukuliwa endapo hawataheshimu makubaliano .

Kulingana na taarifa kutoka Pretoria, ujumbe wa SADC kwa waasi wa FDLR unawataka kuheshimu makubaliano na kutojihusisha na harakati zozote za kijeshi, lakini pia kuendelea kujisalimisha kwa hiari, wakati huu tume ya uchunguzi ikutumwa na ambaya itatowa ripoti katika kikao kijacho cha SADC kuhusu wapi umefikia mchakato huu.

Aidha, Jumuiya ya SADC pia imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuanzisha mchakato wa kuhamishwa kwa mpango wake katika nchi za nje ya ukanda wa Maziwa Makuu kwa ajili ya waasi wa FDLR ambao hawatataka kurejea kuishi nchini Rwanda.

Tangu mwaka 1994, waasi hao wanapatikana katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini ambapo baadhi ya waasi hao wanatafutwa na Mahakama ya kimataifa kwa ushiriki wao katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.

Hata hivyo, tangu watangaze nia yao ya kujisalimisha kwa hiari, ni takriban wassi wa FDLR 200 tu ndio ambao wamejisalimisha pamoja na wanawake na watoto wasiopungua idadi ya watu wapatao 1,500 hadi 2,000, na hivi kukwamisha mchakato kwa muda wa miezi mitatu sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.