Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: upinzani waandamana

Nchini Burkina Faso, mamia ya waandamanaji wamekabiliana na polisi jijini Ouagadougou kupinga rais Blaise Compaoré kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30.

Maefu ya raia mjni Ouagadougou waliandamana, Agosti 23 mwaka 2014.
Maefu ya raia mjni Ouagadougou waliandamana, Agosti 23 mwaka 2014. AFP PHO/ ROMARIC HIEN
Matangazo ya kibiashara

Ibara ya 37 ya Katiba ya Burkina Fasso hamruhusu rais kugombea baada ya mihula miwili kama ilivyo sasa kwa rais Blaise Compaoré na ambapo siku ya Alhamisi

Upinzani nchini humo unasema rais Campaore amekuwa akiendeleza mapindukuzi ya kikatiba ili kuendelea kuwa madarakani.

Shule na vyuo vikuu vimefunga katika miji mbalimbali ili kuendeleza maandamano hayo ya wiki moja kupinga rais Compaoré ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 27 sasa kuwania tena urais mwaka ujao.

Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Benewende Sankara wameapa kuendeleza maandamano hayo.

Wabunge wa nchi hiyo wanatarajiwa kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo.

Hayo yanajiri wakati ambapo vyama vya upinzani nchini Burkina Fasso vimeandaa maandamano makubwa Jumanne Oktoba 28 kupinga marekebisho ya katiba ambayo yanatafsiriwa na wanasiasa wa nchi hiyo na wadau wengine kuwa ni mbinu ya kumruhusu rais Blaise Compaoré kuendelea kubaki madarakani.

Rais Blaise Compaoré yuko madarakani kwa muda wa miaka 27 sasa, na amekua akijaribu kurekebisha baadhi ya Ibara ambazo hazimruhusu kugombea kwa muhula mwengine.

Badhi ya wakaazi wa mji wa Ougadougou wameelezea kutounga mkono mbinu hiyo inayotumiwa na upinzani, wakibaini kwamba upinzani ungelitumia njia nyingine ya kushawishi wabunge wasipitishe muswada huo wa sheria.

Jumatatu Oktoba 27, mamia ya wanawake kutoka vyama vya siasa na mashirika ya kiraia waliingia mitaani na kuandamana wakipinga marekebisho ya Ibara ya 37 ya Katiba ya Burkina Faso, ambayo hamruhusu rais Blaise Compaoré kugombea kwa muhula mwengine. Wanawake hao wameandamana wakiwa na miko mikononi, huku wakiimba nyimbo zinayoikashifu serikali. Wanawake hao wameiomba serilkali kuondoa Bungeni muswada huo wa sheria.

“ Tumejitokeza mitaani tukiwa na miko ili kumuonya mtu huyo ambaye lengo lake ni kuliweka hatarini taifa la Burkina Faso”, ameeleza Juliette Congo naibu kiongozi wa chama cha upinzani MPP, akibaini kwamba kura ya maoni na marekebisho ya Katiba vitasababisha Burkina Faso inaingia katika dimbwi la machafuko.

“ Tumeamua kumwambia rais Compaoré kwamba tunamheshimu kama rais, lakini hatukubaliane naye. Na miko hii ni onyo kwake. Iwapo Blaise Compaoré hatobadilisha uamzi wake kuanzia usiku wa Jumanne Oktoba 28, wanawake wa Burkina Faso watakua kwenye mstari wa mbele kwa kuandamana wakipinga uwezekano wowote wa kuifayia marekebisho Katiba”, ameongeza Juliette Congo.

Idadi kubwa ya askari polisi iliyowekwa mitaani ili kuzuia maandamano hayo haikukataza wanawake hao kuandamana wakianzia katika jengo la Bunge hadi makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mjini Ouagadougou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.