Pata taarifa kuu
TANZANIA-BUNGE-UFISADI-SIASA

Tanzania: mjadala mkali watazamiwa kuibuka Bungeni

Bunge nchini Tanzania linatarajiwa kusikia leo Alhamisi Novemba 27 majibu ya upande wa serikali kuhusu kupotea kwa kiasi kikubwa cha fedha kinachofikia Shilingi bilioni 306 toka akaunti ya Tegeta Escrow.

Mji wa  Dar es Salaam, nchini Tanzania, kilomita zaidi ya 250 kufika Dodoma ambapo kunapatikana majengo ya Bunge la tanzania.
Mji wa Dar es Salaam, nchini Tanzania, kilomita zaidi ya 250 kufika Dodoma ambapo kunapatikana majengo ya Bunge la tanzania. Getty Images/Ariadne Van Zandbergen
Matangazo ya kibiashara

Jumatano Novemba 26, Kamati ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ya hesabu za serikali na mashirika ya umma nchini Tanzania PAC iliwasilisha taarifa yake bungeni kuhusu uchunguzi uliofanywa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow na kupendekeza kujiuzulu kwa waziri mkuu na mwanasheria wa serikali.

Taarifa hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na gamu sio tu na wabunge lakini na wananchi wa Tanzania kutokana na kuhusisha upotevu wa kiasi kikubwa cha fedha kinachofikia bilioni 306 toka akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa kwa pamoja na shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco na kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL.

Akisoma mapendekezo ya kamati yake, makamu mwenyekiti, Deo Filikunjombe ameliambia bunge kuwa kutokana na ushahidi wa walioupata na mahojiano na baadhi ya wahusika, kuna kila haja ya waziri mkuu Mizengo pinda kujiuzulu nafasi yake kutokana na kufumbia macho fedha hizi kuchotwa.

Awali akianza kusoma taarifa ya kamati yake, mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Zuberi Kabwe, aliliambia Bunge kuwa kauli zilizotolewa na waziri mkuu, mwanasheria wa serikali na waziri wa nishati na madini kuwa fedha hizi hazikuwa za umma ni uongo kwakuwa uchunguzi wa kamati yake umebaini bila shaka kuwa zilikuwa ni fedha za umma na akaeleza jinsi zilizvyohamishwa kutoka kwenye akaunti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.