Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-NKANDLA-UJENZI-UFISADI

Mvutano waendelea kujitokeza kuhusu makaazi ya Zuma Nkandla

Suala la makazi ya Jacob Zuma na sehemu zingine za kifahari viliyojengwa katika eneo la Nkandla na kampuni moja Afrika kusini limeibua mjadala.

Makazi ya rais Jacob Zuma katika eneo la Nkandla
Makazi ya rais Jacob Zuma katika eneo la Nkandla REUTERS/Rogan Ward/Files
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma hili kuna taarifa ambazo zimesema kuwa mmiliki wa kampuni ya ujenzi iliyojihusisha na shughuli za ujenzi wa boma la pili la rais wa Afrika Kusini alishtakiwa kwa kosa la udanganyifu na rushwa.

Madai haya hayana uhusiano wa moja kwa moja na shughuli za ujenzi katika eneo la Nkandla, lakini katika miradi mingine iliyofadhiliwa na Wizara ya kazi za Umma.

Mmiliki huyo Thandeka Nene, ambaye ni mwanamke tajiri mwenye umri wa miaka 42Mfanyabiashara tajiri Thandeka Nene,mwenye umri wa miaka 42, alibahatika kupitia kampuni yake Bonelena Construction kujizolea mabilioni ya pesa. Kampuni yake ilichaguliwa kuendesha shughuli za ujenzi wa boma la rais Zuma katika eneo la Nkandla mwaka 2012, mkataba wenye thamani ya Euro 6,500,000.

Lakini Thandeka Nene kwa leo anashtakiwa kushindia zabuni kadhaa kinyume cha sheria, mikataba ambayo imepelekea kampuni yake kunufaika Euro 13,000,000. Inadaiwa kuwa mwekezaji huyo wa Afrika Kusini alinufaika kutokana na makosa ya watendaji wa Wizara ya Kazi za Umma, ambao wamepokea rushwa kubwa kutoka kampuni hiyo. Mwekezaji anatuhumiwa pia ukwepaji wa kodi, na kusema uongo kuhusu shahada zake.

Hakika Thandeka Nene hatuhumiwi kwa kazi kampuni yake iliyofanya Nkandla, lakini ushiriki wa kampuni yake katika miradi iliyoleta utata ambao ulipelekea polisi kuwa makini. Thendeka Nene aliachiliwa kwa dhamana ya Euro 2000, na anatakiwa kujibu mashtaka 18 yanayohusiana na udanganyifu pamoja na rushwa.

Wiki iliyopita, kazi mpya ilifanyika katika boma la Nkandla hususan kukarabati uzio wa umeme kwa uliyogharimu Euro 450 000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.