Pata taarifa kuu
SENEGAL-AFRIKA-MKUTANO-USALAMA-AMANI

Mkutano kuhusu usalama na amani waendelea Dakar

Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika ambao umeanza Jumatatu Desemba 15 umeendelea Jumanne Desemba 16 katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Mkutano wa kimataifa wa amani na usalama umezinduliwa Desemba 15 mwaka 2014 katika jumba la mikutano la hoteli King Fahd, mjini Dakar, Senegal.
Mkutano wa kimataifa wa amani na usalama umezinduliwa Desemba 15 mwaka 2014 katika jumba la mikutano la hoteli King Fahd, mjini Dakar, Senegal. RFI/Tirthankar Chanda
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 350 wakiwemo marais, viongozi wa serikali mbalimbali, Mawaziri wa ulinzi, watafiti na wawakilishi wa mashirika mbalimbali wanashiriki mkutano huo, ambo wengi wanadhani utaleta mabadiliko chanya katika sekta ya usalama.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa jitihada za Ufaransa na Senegal, utakua ukifanyika kila mwaka na utachangia kuunda utamaduni mmoja wa usalama barani Afrika.

“ Natangaza kufungua mkutano wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika”, ni kwa kauli hiyo ya Waziri wa mkuu wa Senegal, Mahammed Dionne, ambayo ilifungua shughuli za mkutano huo, ambao ulianza tangu Jumatatu Desemba 15 na unatazamiwa kuendelea hadi Jumanne Desemba 16 jioni katika jumba la mikutano la hoteli Mfalme Fahd mjini Dakar.

Lengo la mkutano huu ni kuwahimiza viongozi wa Afrika kuhusu ongezeko la wanajihadi katika maeneo ya kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian anashiriki mkutano huu pamoja na marais wengi kutoka bara la Afrika.

Katika hotuba yake kamishna wa taasisi ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya amani na usalama, Smain Chergui, alikumbusha wajibu kwa Afrika na raia wa Afrika kwa kuwa makini kuhusu suala la usalama barani Afrika.

“ Afrika inaweza kua kitovu cha uchumi duniani iwapo tutawajibika kuzidisha juhudi katika sekta ya usalama na kuheshimu haki za binadamu”, amesema Smain Chergui,

Baadaye Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, alipata fursa ya kuelezea wale wote ambao wamekua wakitiwa mashaka kuhusu ufaransa kuwa na majukumu ya kulinda usalama Afrika. Jean-Yves Le Drian amekaribisha mchango mkubwa unaotolewa na kikosi cha Umoja wa Afrika kwa kurejesha amani na usalama katika baadhi ya mataifa barani Afrika.

“ Sudani, Somalia na kwingineko, ni sauti ya Umoja wa Afrika ambayo imekua ikisikika”, ameendelea kusema Waziri wa ulinzi wa Ufaransa.

Jean-Yves Le Drian amebaini kwamba Ufaransa inachangia katika jitihada hizo kwa kuimarisha usalama barani Afrika. Suala la usalama linawahusu kwa njia moja ama nyingine raia wa Afrika wenyewe.

Waziri wa ulinzi swa Ufaransa amezungumzia pia kuhusu hali inayojiri nchini Libya. Amesema kutiwa wasiwasi na tishio la mdororo wa usalaama unotokea kusini mwa Libya.

Jean-Yves Le Drian, amezungumzia pia tishio la kundi la Boko Haram, akibaini kwamba kwa sasa Boko haram si tishio tu kwa Nigeria au kanda nzima, ni tishio kwa ulimwengu mzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.