Pata taarifa kuu
GAMBIA-MAPINDUZI-SIASA

Jaribio la mapinduzi lafeli Gambia

Jeshi nchini Gambia linasema limefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi siku ya Jumanne, jaribio ambalo limekashfiwa na serikali ya Marekani.

Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, akivaa nguo nyeupe na kofia yake ya milele , katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25 mwaka 2014.
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, akivaa nguo nyeupe na kofia yake ya milele , katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 25 mwaka 2014. AFP PHOTO/Don Emmert
Matangazo ya kibiashara

Jaribu hilo lilitokea jana Desemba 30 mwaka 2014 wakati rais Yahya Jammeh mwenye umri wa miaka 49 akiwa ziarani Dubai.

Duru rasmi zasema kuwa watu watatu wanaosadikiwa kuwa wanajeshi na kiongozi wao waliojaribu kutekeleza mapinduzi hayo katika Ikulu ya Banjul wameuawa.

Serikali ya Marekani kupitia naibu msemaji wa Wizara ya mambo ya nje, Jeffrey Rathk, imeshtumu jaribio hilo na kuwataka raia wake kuepuka kutembea jijini Banjul hadi pale utulivu utakaporejea.

Serikali haijazungumzia kuhusu tukio hilo isipokuwa kuwataka wananchi wake kuwa watulivu kwa vile amani na utulivu vipo nchini humo kinyume na uvumi uliopo, huku vyanzo kadhaa vikibainisha kwamba rais huyo amekwenda nchini Ufaransa kwa ziara binafsi.

Hata hivyo duru za kuaminika zimebaini kwamba rais wa Gambia Yahya Jammeh anajiandaa kurejea nchini akitokea Chad, ambapo anapumzika kwa masaa kadhaa, akitokea Dubai.

Rais Yahya Jammeh ameongoza nchi ya Gambia kwa kipindi cha takriban miaka 20, ambapo kwa sensa ya hivi karibuni nchi hiyo ina idadi ya watu wapatao milioni mbili, ikizungukwa na Senegal kama ukanda wa pwani ya Atlantiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.