Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-UCHAGUZI-SIASA

Mvutano wa kisiasa wandelea kujitokeza DRC

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unataka kutolewa kwa kalenda ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha UNC Vital Kamerhe amekosoa hotuba ya kuukaribisha mwaka ya rais Joseph Kabila aliyetangaza kuanzishwa hivi karibuni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, majimbo na manispaa pamoja na sensa ya idadi ya watu.

Vyama hivyo vinasema kuwa kutotaja uchaguzi wa rais mwaka 2016 hakueleweki.

Kwingineko, Naibu Waziri mkuu aliye pia Waziri wa mambo ya ndani, Evarist Boshab anatarajiwa kuwasili hii leo mjini Lubumbashi ambapo maafisa kadhaa wa polisi mjini humo wameitishwa kujieleza ni kwa nini wameshindwa kuzuia mkutano mkubwa wa kumpokea gavana Moise Katumbi, huku wengine wakidaiwa tayari kupoteza nafasi zao kwa sababu hiyohiyo.

 Wakati hayo ya kijiri,Daktari Denis Mukwege ambaye anafahamika kwa kutoa huduma kwa wanawake waliobakwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amelaani hatua ya kufungwa kwa Akaunti za kifedha za kituo chake cha afya.

Mukwege ambaye alipata hivi karibuni tuzo ya kimataifa kwa jitihada hizo amesema kufungwa kwa akaunti ya hospitali ya Panzi mjini Bukavu haikubaliki na kueleza ni usumbufu ambao hauna msingi.

Mwanzilishi wa Hospitali hiyo amesema, serikali imefunga akuanti ya hosptali hiyo kwa tuhuma kuwa anakwepa kulipa kodi na kueleza kuwa, kituo hicho cha afya sio cha serikali, hatua ambayo imesababisha zaidi ya wafanyazi 500 wa hospitali hiyo kutopata mishahara yao.

Kwa miaka 15 hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma kwa wanawake wanaodhulimiwa kimapenzi na kubakwa na waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.