Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHAGUZI-USALAMA

Raisi wa Nigeria Jonathan apuuzia madai ya Obasanjo

Raisi wa Nigeria Goodluck Jonathan amepuuzilia mbali madai ya raisi wa zamani Olusegun Obasanjo kwamba raisi Jonathan ana mpango wa kubadilisha tena tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan analaumiwa kwa kutowajibika kukomesha machafuko kaskazini mwa Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan analaumiwa kwa kutowajibika kukomesha machafuko kaskazini mwa Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya ikulu ilieleza kuwa Obasanjo amemtuhumu raisi Jonathan huko katika mji wa kusini magharibi Abeokuta kuwa kiongozi wa taifa hilo ana mpango wa kufanya kila liwezekanalo ili kupata ushindi katika uchaguzi huo hata kuliingiza taifa katika mgogoro ikiwa hatashinda uchaguzi huo.

Taarifa ya ikulu ilikanusha madai ya Obasanjo kuwa raisi Jonathan hana mpango kama huo na ataendelea kuunga mkono tume huru ya uchaguzi ya Nigeria kuhakikish akwamba uchaguzi ujao unafanikiwa.

Taarifa ya ikulu imebainish akuwa madai ya Obasanjo hayana ukweli kwani yeye ndiye anayepanga kuzua mzozo nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.