Pata taarifa kuu
UNSC-BURUNDI-SIASA-USALAMA

Jumuiya ya kimataifa yatathmini hali ya Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litanatazamiwa kukutana leo Alhamisi ili kuzungumzia machafuko yanayoendelea kuikumba Burundi tangu siku kumi na moja zilizopita.

Maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza yanaendelea Bujumbura.
Maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza yanaendelea Bujumbura. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii, mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki walijielekeza nchini Burundi kwa lengo la kuandaa mkutano wa marais wa jumuiya hiyo utakaofanyika Mei 13 jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo maandamano yanaendelea kushuhudiwa mjini Bujumbura na katika baadhi ya mikoa, huku hati za kukamatwa kwa viongozi wa muungano unaopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza zikiwa zimetolewa.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, balozi wa Tanzania Bernard Membe, amesema kuwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki hazipaswi kuwalazimisha raia wa Burundi kufanya kile ambacho ni kinyume na matakwa yao, huku akibaini kwamba ujumbe wa jumuiya ya Afrika Mashariki ulikuja Burundi kuangalia kinachoendelea.

Mapema, mawaziri walikutana na Rais Pierre Nkurunziza. Ikiwa ni ziara ya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa marais utakaofanyika Mei 13 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Baada ya kukutana na mawaziri, mmoja wa wapinzani walioalikwa, Audifax Ndabitoreye, alikamatwa kabla ya kuachiliwa huru baadaye jioni. " hali hii haitosaidia chochote katika mazungumzo", amesema mmoja kati ya mabalozi wa nchi za Magharibi. wakati huo huo, kwa mujibu wa chanzo cha Umoja wa Mataifa, kwa mara ya pili, viongozi, vyama vya siasa na asasi za kiraia walikutana kwa mazungumzo katika majengo ya Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura.

Hayo yakijiri rais Pierre Nkurunziza amelihutubia taifa Jumatano jioni ambapo amesema amekaribisha uamzi wa Korti ya Katiba ya kumruhusu kuwania muhula wa tatu huku akibaini kwamba iwapo atachaguliwa itakua ni mara ya mwisho kuongoza taifa la Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.