Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Jeshi la Chad laendesha mashambulizi dhidi ya Boko Haram

Jeshi la Chad limeedesha mashambulizi Jumatatu Julai 27 dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram karibu na mji wa Baga Sola kwenye pwani ya Kaskazini mwa ziwa Chad. Mashambulizi haya ni kama majibu ya mashambulizi ya Boko Haram tangu Jumamosi katika visiwa vya ziwa Chad.

Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015.
Maeneo yaliyo pembezoni mwa ziwa Chad yameendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram, kama kijiji hiki cha Ngouboua, mwezi Aprili mwaka 2015. AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi jualai 25, wapiganaji wa Boko Haram waliana kwa kulizingira jeshi, huku wakiendesha mashambulizi katika vijiji vingi ikiwa ni pamoja na Medi, Blarigi na katika kisiwa cha Fitiné, ambapo raia waliyahama makaazi yao.

Lakini kwa kila jaribio, wapiganaji wa Boko Haram walikua wakirudishwa nyuma na jeshi la Chad. Baada ya kuona kuwa wameshindwa, waliamua kuua watu na kuteketeza vijiji kwa moto. Jumatatu wiki hii, wapiganaji wa kundi la Boko Haram walionekana kwenye umbali wa kilomita ishirini na kusini mwa kijiji cha Baga Sola.

Urushianaji risasi ulidumu hadi Jumatau jioni. Mpaka sasa haijajulikana hasara ya mapigano hayo. Hata hivyo katika mapigano hayo, wapiganaji wa Boko Haram walilazimika kurejea nyuma, huku wakiwateka zaidi ya watu thelathini, na mpaka Jumatatu jioni hatma ya watu hao ilikua bado haijajulikana.

Wasiwasi kuhusu muswada wa sheria dhidi ya ugaidi

Mashirika yanayotetea haki za binadamu na vyama vya wafanyakazi vina wasiwasi na muswada wa sheria dhidi ya ugaidi. Katika hali ya kupamana na dhidi ya ugaidi, serikali ya Chad imependekeza muswada wa sheria dhidi ya ugaidi, ambayo mashirika na vyama hivyo vimeitaja kuwa ni sheria ya ubabe, huku vikiomba Bunge kutopitisha sheia hiyo.

Juma lililopita upinzani ulipinga sheria hiyo ambayo viliitaja kuwa inakwenda kinyume na haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.