Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAUAJI-USALAMA

Burundi: raia wengi wauawa katika makabiliano na polisi

Nchini Burundi, zaidi ya raia kumi na tano wameuawa katika makabiliano na polisi Usiku wa Jumamosi kuamia Jumapili mwishoni mwa wiki hii.

Polisi katika kata ya Cibitoke, mwezi Mei, 2015. Kata hii imeshihudia makabiliano makali mwishoni mwa juma hili kati ya raia na vikosi vya usalama.
Polisi katika kata ya Cibitoke, mwezi Mei, 2015. Kata hii imeshihudia makabiliano makali mwishoni mwa juma hili kati ya raia na vikosi vya usalama. AFP PHOTO/PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Yote yalianza siku ya Jumamosi mchana wakati polisi iliendesha msakao na kuanza kuwakamata watu mbalimbali hasa vijana wanaopinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunzizakatika kata ya Mutakura, wilayani Cibitoke, kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Makabiliano yalienea katika maeneo ya Cibitoke, Kamenge na Ngagara. Mashahidi wamesema kuwa zaidi ya watukumi na tano wameangamia katika makabiliano hayo, huku wakiinyoshea kidole cha lawama polisi, hasa kikosi cha kuzima ghasia kiliyoundwa hivi karibuni.

Hii ni baada ya miili ya watu kupatikana mabarabarani na wakaazi wa vitongoji vya Bujumbura.

Mashirika mbalimbali ya kimataifa yamebaini kwamba wawakilishi wao wameona maiti barabarani katika mitaa ya kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Mashirikia hayo yamebaini kwamba, baadhi ya wahanga hao wamepigwa risasi kichwani, na inaelekea walifungwa kwa kamba kabla ya kuuwawa.

Msemaji wa polisi, Pierre Nkurikiye, amewalaumu wahalifu kwa vifo hivyo, akibaini kwamba yote hayo yanasababishwa na wao.

Miili 6 ilionekana katika kitongoji cha Cibitoke, ambacho kimekuwa shina la maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.